Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo.
Goodluck Ngai na Nassor Gallu
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo, amewaandaa viungo washambuliaji Mrisho Ngassa na Simon Msuva kuwa ndiyo chachu kubwa ya ushindi wake dhidi ya watani wao wa jadi Simba, katika mchezo wao wa Oktoba 18, kwenye Uwanja wa Taifa.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo, amewaandaa viungo washambuliaji Mrisho Ngassa na Simon Msuva kuwa ndiyo chachu kubwa ya ushindi wake dhidi ya watani wao wa jadi Simba, katika mchezo wao wa Oktoba 18, kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba na Yanga watakutana katika mchezo wa raundi ya nne wa Ligi Kuu
Bara, huku zikiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1, katika mchezo wao wa
mwisho wa ligi hiyo walipokutana katika uwanja huo msimu uliopita.
Katika mazoezi ya Yanga ambayo yanafanyika kwenye Uwanja wa Boko
Veterani uliopo Boko nje kidogo ya Jiji la Dar, Maximo ameonyesha
kuwatumia zaidi viungo wake hao wenye kasi kupiga mipira ya krosi
kwenda kwa washambuliaji wake wanaoongozwa na Mbrazili, Geilson Santos
‘Jaja’ na kuwapa kazi rahisi ya kupachika mipira wavuni.
Katika mazoezi hayo ya jana asubuhi, Maximo alitumia muda mwingi
kuwapa viungo hao mazoezi maalum ya kupiga krosi zitakazoleta madhara
katika lango la wapinzani wao huku akiwataka washambuliaji kuzitumia
vizuri krosi hizo.
Mbali na Msuva na Ngassa waliolifanya zoezi hilo kwa muda mrefu na
kwa ufasaha mkubwa, Maximo aliwatumia pia wachezaji wengine katika zoezi
hilo ili nao pia wapatapo nafasi ya kupiga krosi wapige zenye madhara.
Wachezaji waliofanya zoezi hilo ni pamoja na Andrey Coutinho, Nizar
Khalfan, Hussein Javu na beki Edward Charles.
إرسال تعليق