Wanawake 40 watekwa nyara Ituri mashariki ya DRC

Wanawake wasiopunguwa 40 wanaripotiwa wametekwa nyara katika Wilaya ya Mambassa, jimbo la Orientale mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaaminika wanawake hao walitekwa na waasi wenye silaha wa kundi linaloongozwa na mtu anaejulikana kwa jina la Manu.
Maafisa wa wilaya hiyo wanahofia kwamba wanawake wamechukuliwa na kupelekwa ndani ya msitu katika ngome ya waasi hao. Wanawake walitekwa katika eneo la kuchimba madini la Bakaiko.
Mkuu wa wilaya ya Mambassa Alfred Bongwalanga anasema kutokana na utekaji nyara unaofanyika katika eneo hilo ana wasi wasi kuna mipango ya kuanzisha tena uwasi huko Mashariki ya Kongo.
Siku ya Jumatatu wakuu wa wilaya waliwataka wananchi wenye silaha zisizo halali kuzisalimisha kwa maafisa wa usalama na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Maraifa huko Kongo, MONUSCO.
Wakati huo kumekuwepo na habari za kutekwa wanaume 12 katika eneo karibu na mapka wa Uganda, lakini hakuna habari zaidi juu ya tukio hilo.

Post a Comment

أحدث أقدم