Kyela. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu imesema kuwa haitapitisha bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa
kile kilichoelezwa kubaini uozo wa ujenzi usiokidhi kiwango katika
miradi ya miundombinu ya barabara wilayani Kyela mkoani Mbeya, ikieleza
kwamba italazimika kutembea nchi nzima ili kujiridhisha na miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa juzi katika majumuisho ya
ziara ya kamati hiyo iliyoongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe iliyotembelea Bandari za Itungi na Kiwila kujua shughuli
mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea.
Wakiwa njiani, msafara huo ulisimamishwa mara tatu na wananchi na wengi wakieleza kero yao kuwa ni ubovu wa miundombinu.
Akizungumza katika ziara hiyo, mbunge Viti
Maalumu, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Maryam Msabaha alisema kuwa
kitendo kilichotokea wilayani Kyela ni cha aibu na kwamba kamati hiyo
haitavumilia uozo huo unaofanywa na wizara na halmashauri kushindwa
kusimamia kikamilifu makandarasi wanaopewa zabuni na kusababisha
Serikali kushushiwa mzigo wa lawama.
“Magufuli ni jamaa yangu, sitasita kumweleza
ukweli na kwamba bajeti yake haiwezi kupitishwa bila kamati hii
kuzunguka nchi nzima ili kujiridhisha na miradi ya ujenzi wa
miundombinu. Anapaswa kutambua fedha zinazotumika katika miradi hiyo ni
kodi za wananchi na ni haki yao kulalamika,” alisema
Post a Comment