Katika hali isiyotarajiwa na wengi karibu viongozi wote wa vyama
vya siasa wakiwamo wa Chama tawala CCM waliohojiwa kuhusu uchaguzi wa
Serikali za Mitaa, wamelalamikia uchaguzi huo na kuainisha kasoro
mbalimbali zilizochangia kuvuruga kazi hiyo yote.
Baadhi ya kasoro hizo ni pamoja na kukosekana kwa
majina ya wapiga kura, majina ya wagombea kujichanganya na nembo za
vyama kuwekwa tofauti.
Kasoro zingine ni kuchelewa kuanza kwa uchaguzi
huo, majina ya watu kutumika kupigiwa kura na wasiohusika na mengine
kuonekana katika vituo viwili tofauti.
Kutokana na kasoro hizo, CCM wanasema walilazimika
kuwashauri baadhi ya vingozi wake washinikize kuahirishwa kwa uchaguzi
huo kutokana na wingi wa kasoro.
CCM
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
anasema kwa ujumla uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi ikiwamo ya
ucheleweshwaji wa vifaa katika vituo vya kupigia kura.
Anaongeza kuwa hali ilivyoonekana kuzidi kuwa na
utata waliwashauri viongozi wa vyama vyao kushinikiza baadhi ya maeneo
uchaguzi huo uahirishwe.
“Kwa kweli kuna dosari nyingi, kuna baadhi ya
vituo vilikosa vifaa muhimu ikiwemo wino ambao sisi tuliamini ungeweza
kuwadhibiti watu waliojiandikisha zaidi ya mara tatu, tulibaini miongoni
mwa watu hao ni wa Chadema,” alisema.
Nnauye anasema kasoro nyingine ambayo waliibaini
ni karatasi za kura zilikuwa zimegeuzwa nembo za vyama, picha na jina ni
la mgombea wa CCM lakini nembo inawekwa ya Chadema.
“Pia kuna sehemu nyingine vijana wa Chadema walijipanga kwenye njia za kuelekea kwenye vituo na kuwatishia wapiga kura.
“Tatizo hilo la udanganyifu nafikiri tunaweza
kulidhibiti kwa kuwa na vitambulisho vya pamoja, ingawa pia limetimia
kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya mawakala,” anasema.
Anaendelea kusema hata hivyo kuna haja kwa
Serikali kuwaadhibu haraka iwezekanavyo wale wote ambao walihusika
kusababisha uchaguzi kuwa na kasoro zilizosababisha vurugu katika baadhi
ya maeneo.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment