TWIGA STARS YAANZA 'VIBAYA
![]() |
| Twiga Stars |
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza ‘vibaya kidogo
kampeni za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa
wanawake, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni hii mjini Addis Ababa na wenyeji,
Ethiopia.
Twiga sasa inahitaji ushindi wa 1-0, Juni 16, katika mchezo
wa marudiano mjini Dar es Salaam, ili kukata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa
mara ya pili mfululizo, Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane
katika historia ya michuano hiyo.

إرسال تعليق