Waziri wa Usalama wa ndani
Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika
ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la
Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji
mkuu wa Nairobi.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyi

إرسال تعليق