*Mwenyekiti wa Bunge adai Spika amefunga mjadala wake
*Wabunge wachachamaa, wataka mgomo ujadiliwe
*Dk. Hussein Mwinyi apigilia msumari wa mwisho
KITENDO cha kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, kimeonekana wazi kulivuruga Bunge, baada ya wabunge kuzuiwa kujadili mgomo wa madaktari unaoendelea.
Agizo hilo, lilitolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi).
Katika mwongozo wake, Mkosamali alisema kuna haja Bunge kusimamisha shughuli zake kwa muda na kujadili mgomo huo, kwa kuwa siyo busara Bunge kuendelea na kazi wakati baadhi ya Watanzania wanaendelea kupoteza maisha kutokana na kukosa matibabu.
Kutokana na kauli hiyo, Mkosamali aliwaomba wabunge wenzake, wamuunge mkono, jambo ambalo walilifanya wakionyesha kukubaliana na hoja yake.
Hata hivyo, Jenista ambaye ni Mbunge wa Peramiho (CCM), alisema hakuna haja wabunge kuendelea na mjadala huo kwa kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, alishauhitimisha.
“Suala la mgomo wa madaktari, limeshatolewa ufafanuzi na Spika, kwa hiyo, hatuwezi kuendelea nalo hapa kwa sababu tukifanya hivyo tutakuwa tunakiuka Kanuni za Bunge.
“Lakini, kama kuna mbunge ambaye hakuridhika na uamuzi wa Spika, anaweza kulileta jambo hili kwa njia nyingine na Spika ataangalia kama kuna umuhimu wa kulijadili.
“Kwa hiyo, hata wewe Mheshimiwa Mkosamali kuomba Mwongozo wa Spika katika jambo unalojua limeshatolewa ufafanuzi na Spika, umekiuka Kanuni za Bunge,” alisema Jenista.
Pamoja na kutoa ufafanuzi huo, Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo (CCM), alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Rais ya mwaka wa fedha wa 2012/2013, aliendelea kuzungumzia mgomo huo.
Katika mchango wake, Jafo alisema kuna haja uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, kufanyika haraka iwezekanavyo, ili ukweli uweze kujulikana.
Kwa mujibu wa Jafo, kuna uwezekano kwamba, Dk. Ulimboka alitekwa na kujeruhiwa na watu wanaotaka kuipaka matope Serikali, jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua ukweli wake.
Baada ya Jafo kugusia tena mgomo wa madaktari wakati wabunge wameshazuiwa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), alisimama na kusema taarifa, lakini hakuruhusiwa kuzungumza kwa kile kilichoelezwa na Jenista, kuwa alikiuka Kanuni za Bunge.
Jafo, alipomaliza kuchangia mada hiyo, ilifika zamu ya Mbunge wa Chake Chake, Mussa Haji Kombo (CUF), ambaye naye alianza kuzungumzia mgomo huo na kusema hakuna haja ya kuujadili kwa kuwa madaktari wamesharudi kazini.
Kauli hiyo ilimfanya Mnyika asimame tena na kusema taarifa na aliporuhusiwa, alisema mgomo haujakwisha na kwamba vyombo vya habari vya jana, viliwakariri baadhi ya madaktari, wakiwamo madaktari bingwa, wakisema hawako tayari kurudi kazini.
Pamoja na hayo, Mnyika alitaka kujua ni kwa nini jambo lililozuiwa na Mwenyekiti wa Bunge linaendelea kujadiliwa bungeni.
Akitoa ufafanuzi wa mwongozo huo, Jenista alisema alizuia wabunge kujadili suala hilo kwa kuwa jana (juzi) lilizusha mjadala mzito, lakini Jafo na Kombo walikuwa na haki ya kulizungumzia kwa kuwa walikuwa wakilijadili kwa ustaarabu.
Jenista alipomaliza kusema hayo, Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), alisimama na kusema Bunge haliwezi kuendeshwa kwa kufuata vyombo vya habari vimesema nini, badala yake linaongozwa kwa mujibu wa Kanuni.
Mjadala huo, ulizidi kushika kasi, ambapo Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (CHADEMA), naye alisimama na kusema taarifa aliyopewa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mgomo huo, imepotoshwa. Kutokana na hali hiyo, alitaka ripoti ya mazungumzo kati ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Serikali iliyohusu mgomo wa madaktari, iwasilishwe bungeni ili wabunge wajue ukweli wa mgomo huo.

Chanzo:- Mtanzania
إرسال تعليق