SIMBA WAIPIGIA MAGOTI AZAM KWA REDONDO, WATOA MILIONI 15 YAISHE WABEBE KIFAAA

SIMBA WAIPIGIA MAGOTI AZAM KWA REDONDO, WATOA MILIONI 15 YAISHE WABEBE KIFAAA

Redondo
YAMEKWISHA. Naam, sasa Simba SC na Azam FC ni amani tupu. Azam imekubali kupokea Sh. Milioni 15 kutoka Simba SC ili kumuuza kiungo wake, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa Wekundu hao wa Msimbazi.
Habari za ndani ambazo Chanzo imezipata, zimesema kwamba hiyo inafuatia viongozi wa Simba SC kuwaangukia Azam kwa kitendo chao cha kumsajili kiungo huyo bila kuwasiliana nao, wakati bado alikuwa ana mkataba na Wana Lamba Lamba.
Awali, Azam walikerwa na kitendo hicho hadi wakataka kusitisha dili la kumtoa kwa mkopo kwa Mrisho Khalfan Ngassa Simba SC. Chanzo:- http://bongostaz.blogspot.com/
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa, baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi uliopita.
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
Inavyoonekana, Redondo aliwadanganya Simba kwamba amemaliza mkataba na Azam, wakaingia mkenge na kumpa Sh. Milioni 30 wakimsainisha mkataba wa miaka miwili, wakati mkataba wake na Azam unamalizika Juni mwakani.
Hili ni kosa sawa na ambalo Simba walilifanya katika usajili mwingine wa mchezaji wa Azam, Ibrahim Rajab ‘Jeba’, miezi mitatu iliyopita ambaye alikuwa kwa mkopo Villa Squad wao wakaenda kumsajili bila kuwasiliana na klabu yake kujua kuhusu mkataba wake, matokeo yake baadaye mchezaji huyo akarejea Azam.
Simba nao wana lalamiko kama hilo, dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga wanaowatuhumu kumsajili beki Kevin Yondan, wakati bado ana makataba na Wekundu hao wa Msimbazi, ingawa TFF iliweka sawa kwa kusema Yondan hakuwa na mkataba na Simba SC.
Baadaye Simba ilitoa ufafanuzi, kwamba ilimuongezea mkataba Yondan baada ya ule wa awali kumalizika na ikawa inasubiri muda wa usajili ufike wauwasilishe TFF. Lakini katika kesi ya awali, Simba walipoupeleka mkataba wao mpya na Yondan, ulionyesha mchezaji huyo anatakiwa kuanza kuutumikia mkataba huo, Desemba mwaka huu, hivyo TFF ikasema kwa wakati ambao yuko huru, aichezee Yanga.
Sakata la Yondan litarudi Desemba, wakati ambao atatakiwa kuanza kuutumikia mkataba wake na Simba, wakati yupo ndani ya mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post