SEKRETARIETI YA CCM YAWASILI SALAMA MKOANI KIGOMA


 
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akimpongeza Dereva wa Treni aliyewafikisha Mjini Kigoma salama, Kambi Ali. Wengine pichani kutoka kushoto  ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye , Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela
Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewasili salama mkoani Kigoma ikitokea jijini Dar es Salaam kwa njia ya Reli.

Wakipokelewa kwa Shangwe, takribani kila kituo njiani, Sekretarieti hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana pamoja na wajumbe wengine ambao ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela uliwasili Mjini Kigoma majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na Wakazi wa mji wa kigoma.

Akizungumza baada ya kuwasili Kigoma, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alisema yakuwa leongo la safari yao hiyo ya Treni ni kuwadhihirishia wakazi wa Kigoma na taifa kwa Ujumla kuwa Usafiri wa Treni ni wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi kuanzia sasa itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuboresha huduma maradufu na kuhakikisha safari zinaongezeka.

Nao baadhi ya wakzi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wa kusafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi Kigoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwa treni na kudai kuwa kufanya hivyo ni uzalendo tosha na kuonesha haki kwa wananchi wote.
 Katibu Mkuu akizungumza na wananchi wa Kigoma
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia na wananchi wa Kigoma
 Wananchi wakisogea kuwapokea viongozi
 Burudani hii ya ngoma ilikuwepo
 Sekretarieti ikipokea heshima ktoka kwa Chipukizi.
 Chipukizi wakimvisha Skafu Katibu Mkuu wakati wa mapokezi.
 Katibu Mkuu akifurahia ngoma na Katibu wa Itikadina Siasa, Nape akipiga ngoma.
 Kinana akizungumza na wanchi wa Kigoma
 Wananchi wakiwa Stesheni kushuhudia viongozi hao.

Post a Comment

أحدث أقدم