
Dereva wa Lori la Maji wa Kampuni ya Dolfin yenye maskani yake Mbezi
Tang Bovu, jijini Dar es Salaam,ambaye hakuweza kufahamika jina lake
mapema, akiugulia maumivu baada ya kupigwa na kuumizwa na jamaa wawili
waliokuwa na kina dada wawili katika gari ndogo eneo la Mbezi njia
inayoingia katika Shule ya Mbezi Beach Sekondari jana usiku.
Dereva huyu alikuwa akitokea Barabara kubwa akiingia katika njia ndogo
inayoelekea Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach, na gari ndogo ilikuwa
ikitokea katika njia hiyo ndogo na kukutana uso kwa uso na lori hilo,
huku watu waliokuwa katika gari hiyo ndogo wakimtaka dereva wa lori
kuwapisha wao ili waanze kupita.
Dereva huyu aliamua kubana kushoto na kuwaachia njia ili wapite, kama
picha ya Lori inavyoonyesha chini, lakini jamaa waliokuwa katika gari
ndogo waliamua kushuka na kumshusha dereva huyo na kisha kuanza
kumshambulia kwa magumi na mawe, huku dereva huyo akitoka nduki na
kuacha gari lake, hadi katikati ya barabara inayoelekea Tegeta ikitokea
Mwenge, walipomtia mikonini na kuanza kumpiga kama mwizi huku wakitumia
mawe kumpigia kama makwenzi, na kumuumiza kama hivi, hadi walipofika
watu kibao na kuanza kuamulizia ugomvi huku wakijua kuwa jamaa huyo ni
mwizi huku wengine wakijandaa kunza kumshambulia.
Lakini watu hao baada ya kupata stoti kamili ilivyokuwa waliamua
kuwageuzia kibao watu hao wakianza kuwasonga kutaka kuwashambulia ndipo
walipoamua kudandia gari na kukimbia, huku mmoja kati ya wanawake
waliokuwa na jamaa hao, akisikika kumwambia jamaa huyo,
''usirudie kutukana watu waliovaa suti hovyo bila kuwajua watakuua''.
Gari hiyo wakati ikianza kuondoka eneo hilo hukuikiendeshwa na
mwanamama, ilianza kushambuliwa kwa mawe kwa bahati iliwahi kuondoka
eneo hilo na kuingia usawa wa Barabara ya Masana na kutokomea.

Watu hao wakidandia gari iliyoanza kutembea ili kutoweka eneo hilo.

Jamaa hao wakianza kuondoka eneo hilo kwa kasi huku gari hiyo ikiendeshwa na Mwanamama.

Lori lililozua kasheshe hilo, ndiyo hili na eneo lenyewe ndo kama hivi
linavyoonekana huku magari yakiwa na uwezo wa kupita bila kugusana na
lori hilo.

Lori hilo likiwa limeachwa katika eneo la tukio baada ya dereva wake
kupewa kipondo huku magari mengine yakipita kama kawaida.Picha na
Sufiani Mafoto Blog.
إرسال تعليق