Msanii maarufu wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya
Solexx Mgenge a.k.a Gospel King amefunguka kuhusu past yake kuwa alikuwa
addicted kwa kuangalia movie za ngono
Katika interview aliyofanya na mtandao wa zuqka, Solexxx
alikiri kuwa alipokuwa kidato cha tano akiwa na umri wa miaka 11 kuna jirani
yake aliyekuwa anasoma vidato vya juu zaidi alikuwa anaenda kwao na video
cassettes za aina mbalimbali na baadhi zilikuwa ni za ngono na waliangalia
wote.
Solexx alisema alinogewa sana na siku ilikuwa haipiti bila
kuangalia ‘po*n*grap*ic stuff’, screen saver ya laptop yake ilikuwa na picha za
wasichana wakiwa uchi, simu yake pia ilikuwa na wallpapers kibao za ngono.
King of Gospel kama anavyojiita hivi sasa, aliendelea na
hali hii hadi alipofika kidato cha pili ambapo mama yake mzazi aliinasa DVD ya
ngono a.k.a Pilau kwenye begi lake, na hapo akampeleka moja kwa moja kwa
mtaalam wa counseling na kuanza darasa lililomsaidia kidogo, lakini ilikuwa
ngumu kwa sababu washkaji zake kibao bado walikuwa wanaendelea kuangalia movie
hizo na walikuwa wote mara kwa mara.
Mungu alimsaidia kuyavuka haya na ndipo akaanza kuwaza
hasara kubwa aliyokuwa anaipata kwa kufatilia mikanda ya ngono, “niligundua
nilikuwa natumia pesa nyingi sana kudownload po*n*g*aphic stuff, nilikuwa na
zaidi ya 100GB ya moviez za ngono kwenye laptop yangu,” alifunguka.
Lakini mambo yalibadilika kabisa baada ya kuamua kuokoka na
sasa anaishi maisha tofauti, sasa akiwa kama mtu aliyekwa addicted na movie
hizi, huu ndio ushauri wake kwa watu wanaoangalia movie za ngono;
“Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba unapoteza muda mwingi
sana kuangalia, na bado ni useless. Ona, unapoangalia po*n, kinachofuata ni
kujaribu kitu halisi. Hiii ndo sababu wengi wanaacha shule kwa
sababu ya mimba zisizotarajiwa, na HIV/AIDS inasambazwa sana.”
Post a Comment