MSIKILIZE BABU WA LOLIONDO KWENYE HIZI SEKUNDE 40 ZA PROMO YA INTERVIEW YAKE


Alhamisi hii feb7 2013 kuanzia saa moja usiku kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM dakika 120 zitatumika kuirusha Exclusive interview ya BABU WA LOLIONDO, hapa ni wakati nilipofika Loliondo… ni safari iliyochukua dakika 570 kutoka Arusha mjini, ni zaidi ya saa 9.
Safari ya kwenda kwa Babu wa Loliondo Samunge ilianza kesho yake, hapa nilikua kwenye defender ya polisi kwa sababu magari ya watu binafsi yalikua yanagoma kwenda kutokana na vita kali ya Wasonjo na Wamasai, hivyo njia pekee ya kufika kwa Babu ni kusindikizwa na Polisi ambao niliweka mafuta kwenye gari yao, ni safari iliyochukua kama saa 5 kufika sababu njia inayotumika ndio kwenye vita, tulipita eneo la vita, stori kamili ni Alhamisi hii feb 7 2013 kwenye AMPLIFAYA Clouds Fm.
Nikiwa kwenye interview ya zaidi ya dakika 60 na Babu wa Loliondo Ambilikile, pichaz na stori nyingine zitapatikana hapa kwenye millardayo.com kuanzia jumatano usiku na alhamisi, kwa sasa msikilize Babu wa Loliondo kwenye hiyo promo yake hapo chini.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post