WACHEZAJI WA SIMBA NA MAZEMBE KUTINGA KAMBINI LEO,

Wachezaji waliotwa na kocha Kim Poulsein wanao kipiga simba sc na TP Mazembe wanataraji kuungana na wenzao katika kambi ya Taifa stars hii leo.
Wachezaji wa Taifa stars walianza kuwasili kambini jana kwa wachezaji toka Azam fc, mtibwa sugar na yanga na kusalia wachezaji wa simba na TP Mazembe ambao wataingia leo.
Wachezaji wa simba walio itwa katika kikosi cha taifa stars ni Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Saidi Cholo, Mrisho Ngassa na Amir Kiemba.
Wachezaji wa TP Mazembe walioitwa katika kikosi hicho kitakacho wakabili Cameroun february 6 ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.

Wakati huo huo wachezaji wa Cameroun wanatarajiwa kuanza kuwasili leo kwa makundi.

Post a Comment

أحدث أقدم