TTCL YAZINDUA HUDUMA YA ‘BANDO NA TTCL’ NA KAMPENI YA PUNGUZO KUBWA LA BEI YA INTANETI

IMG_6851Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha moja ya simu zinazouzwa na kampuni hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora wakati kampuni hiyo ilipozindua rasmi huduma za Bando na TTCL na Basti  leo jijini Dar es salaam kulia ni Kisamba Tambwe Mkuu wa Mauzo Kampuni ya TTCL. IMG_6852Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha kampeni ya Bando na TTCL mara baada ya kuizindua rasmi kushoto anayepiga makofi ni Ernesti Isaya Mkuu wa Maendeleo ya Bidhaa TTCL. IMG_6856Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha kampeni ya BASTI ambayo ina viwango vipya vya muda wa kuperuzi kwenye mtandao wa kampuni hiyo.

…………………………………………………………………………
TTCL, imezindua huduma  mpya ya Bando Na TTCL inayoambatana na punguzo kubwa la bei kwa huduma ya INTERNET. Mtakumbuka ni Juzi tu tareha 21 Machi 2013 tulifungua kituo chetu kipya cha huduma  kwa wateja kilichopo  Kariakoo katika mkoa wa Dar es Salaam katika kupanua mtandao wa huduma kwa wateja  nchini (>30 CSC network nchini). 
 
Kifuatacho sasa ni kupanua wigo wa huduma kwa wateja. Vilevile mtakumbuka kuwa baada ya kujitambulisha sokoni na huduma ya ‘Mobile Internet’ isiyo na kikomo ya BANJUKA; kampuni ya simu ya TTCL sasa inazindua huduma mpya inayojulikana kama ‘BANDO NA TTCL’. Huduma hii inamuwezesha mteja kufaidika na meseji za bila kikomo, kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa wakati mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500. BANDO NA TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za TTCL (zinazopatikana ktk vituo vya huduma kwa wateja nchini). 
 
Maelezo zaidi ya juu ya huduma hii yanapatikana kwa kupiga 100 huduma kwa wateja au tembelea ofisi zetu za mauzo zilizoenea nchi nzima. Aidha, TTCL imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intaneti zaidi kwa gharama nafuu. Hili ni punguzo la bei la aina yake. Mathalani; kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000 sasa kinauzwa kwa shilingi 25,000 tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo wa TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL. (Haki ya mawasiliano kwa wote)
 
Leo hii, wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiliamali wanatumia simu za kisasa (smart phones, tablet PCs kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti na mitandao ya kijamii kwa mfano, Michuzi blog, facebook twitter, LinkedIn n.k ) kwa shughuli zao za kila siku. Upatikanaji wa vifaa hivi vya kisasa (sambamba na ukuaji wa teknolojia) na kumewezesha kukua kwa kasi kwa tabaka la kati lawatumiaji hivyo kumesababisha kukua maradufu kwa soko la intaneti hapa nchini. (Hili nijambo jema sana kwa nchi yetu na maendeleo ya watu wake kiuchumi na kijamii)
 
Kwa kuzingatia haya (na kutambua kuwa mawasiliano na habari ni swala mtambuka), TTCL ina mikakati wa kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za intaneti na mawasiliano & habari kwa ujumla na hivyo kuwa chachu kubwa ya maendeleo nchini. Huduma mpya ya BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI ni juhudi za makusudi za TTCL katika kutimiza adhma hii.
 
Kwa kifupi huduma za BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI zina manufaa yafuatayo kwa mteja:
 
1. Huduma ya ‘mobile internet’ kwa gharama nafuu
 
2. Vifurushi vya siku, wiki na mwezi kulingana na mahitaji yako
 
3. ‘Mobile Internet’ yenye ubora na kasi ya juu zaidi
 
4. Kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti
 
5. Huduma ya BANDO NA TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones.
 
6. Inakupa thamani bora kwa pesa yako
 
TTCL kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa inalo jukumu kubwa la kutoa huduma za mwasiliano kwa wateja wake nchini na nje ya mipaka yake. Uwepo wa mitandao ya mawasiliano ya baharini ya EASSy na SEACOM katika pwani ya Tanzania, mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mtandao wake ulionenea nchi nzima umeiwezesha TTCL kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za mawasiliano ikiwamo intaneti kwa ofisi za serikali na benki mbalimbali hapa nchini. Mkongo wa Taifa umesaidia kuwa na huduma bora zaidi ambapo kwa sasa wananchi tunaweza kupata huduma nyingi zikiwemo matibabu mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao na Serikali mtandao, Benki – Mtandao, Pesa – mtandao na pia kufanikiwa kuifikisha Tanzania katika nchi za Zambia, Burundi, Rwanda na Malawi kwa huduma za mawasiliano.
 
TTCL itaendelea kupanua wigo wa mtandao na huduma zake kukidhi mahitaji ya mawasiliano na habari ya wateja wake na watanzania wote. Nisisitize tena BANDO NA TTCL pamoja na BASTI imetengenezwa kukidhi mahitaji ya watumiaji wote :- Maofisini, Biashara ,Vyuoni, mashuleni na pia majumbani kwa familia.
 
Huduma ya BANDO NA TTCL inakuwezesha kupata mgezi, kutuma meseji bila kikomo na kuperuzi – Intaneti kupitia simu za mkononi. Kampeni ya BASTI inakupatia punguzo kubwa la bei ya Mobile Intaneti kupitia modemu zinazotumia teknologoia ya kisasa EVDO itolewayo na TTCL. Tumia huduma hizi hakika utafurahia

Post a Comment

Previous Post Next Post