Kufuatia
wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu
marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi
yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja
iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu Kusini na
Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya
maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini Congo.
Wabunge
wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa
kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na
makundi ya waasi wanayopingana nayo.
Wabunge
wa Kivu wametaka pendekezo la Rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele
na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani ya kudumu kwenye eneo hilo.
Mbunge
wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa
hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao
serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.
Akisema
“Rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba
mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali
kupitia mtizamo ulio thabiti. Bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa
serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.
Kwa
muda wa siku tano sasa pendekeo hilo la rais Kikwete limeendelea kuzusha
maoni mengi kwenye vyombo vya habari ngazi ya kisiasa, na kwa watu wa
kawaida huko mjini Kinshasa.
إرسال تعليق