UTATANISHI NA UKIMYA KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA
Issa Shivji
MHADHARA WA KUAGA KIGODA CHA MWALIMU
IGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERKE
Copyright © Issa Shivji, 2013
Kwa dhati
kabisa ningependa kuwashukuru wanakigodawenzangu, Ng’wanza Kamata,
Saida-Yahya-Othman naBashiru Ally, kwa mazungumzo marefu na
mabishanomakali ambayo yamenisaidia kunoa hoja zangu na
kuwazayasiyowazika. Shukrani zangu kwa Walter Rodney Luanda naBashiru
Ally, waliosimamia uchapishaji wa Mhadhara katikamuda mfupi wa siku
mbili. Walter amekuwa bega kwa beganami kwa miaka mitano yote ya
uNyagoda wangu. Amefanyakazi za Kigoda kutokana na imani na msimamo wake
na siokiajira tu.Mwishowe, namshukuru sana, kwa moyo mkunjufu,
SaidaYahya-Othman ambaye amehariri Mhadhara kwa ustadi wamtaalam wa
lugha katika masaa ishirini na nne, tena katikasiku yake ya mapumziko
maalum.
Shukrani
1. Naialika
kaumu, tutafakari pamoja,Kuhusu Tunu muhimu, Rasimu ilizotaja,Kati ya
Tunu adhimu, mojawapo ni umoja,Kabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu2.
Umoja hauwi Tunu, Kwa taifa tegemezi,Bali umoja ni Tunu, baada ya
ukombozi,Umoja hasa ni mbinu, ya kuunda mapinduzi,Kabla ya ukombozi,
Umoja hauwi Tunu.3. Uchumi wa nchi yetu, ni uchumi tegemezi,Na hasa
kilimo chetu, siyo cha kimapinduzi,Na pia elimu yetu, ni chombo cha
ubaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.4. Tanzania nchi yetu, sasa
haina amani,Uhuru na utu wetu, kwa sasa viko rehani,Fikra na mila zetu,
havina tena thamani,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,5. Tutafakari
maoni, ya waliotangulia,Ya Mkwawa na Fanoni, na ya Bibi Titi pia,Umoja
walithamini, hoja waliujengea,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.6.
Umoja imara hasa, siyo uliopo sasa,Huu umoja wa sasa, ni umoja wa
mikasaMikasa ya kisiasa, na hila za wenye pesa,Kabla ya ukombozi, Umoja
hauwi Tunu.7. Umoja si mapatano, baina ya wala tonge,Umoja si mikutano,
ya Jangwani na Kisonge,Umoja ni muungano, wa tabaka la wanyonge,Kabla ya
ukombozi, Umoja hauwi Tunu,8. Umoja sio ubia, wa mitaji ya
‘mabwana’,Umoja ni ujamaa, wa watu wasonyonyana,Umoja kwa wenye njaa, ni
nyenzo muhimu sana,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.9. Mhimili wa
umoja, ni dira ya ukombozi,Na adui wa umoja, ni mifumo kandamizi,Na
kitanzi cha umoja, ni sera za kibaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi
Tunu.10. Tunataka ukombozi, wa fikra za wanyonge,Tunataka mapinduzi, ya
uchumi wa wanyonge,Tunataka mageuzi, ya Umoja wa wanyongeKabla ya
Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
UMOJAHAUWI TUNU,KABLA YAUKOMBOZI
– Na Mwalimu Bashiru Ally
5
UTANGULIZI
Niliposimikwa
mnamo tarehe 18 Aprili 2008 kuwa Profesa waKigoda cha Taaluma cha
Mwalimu Nyerere katika Umajumui waAfrika, nilitoa mhadhara wa uzinduzi
juu ya ‘Umajumui wa Afrikakatika Fikra za Mwalimu’. Sasa ninakaribia
kumaliza muda wanguhapo tarehe 31 Agosti 2013, nimeona si vema
nikiondoka bilakutoa mhadhara wa kuaga Kigoda, wanakigoda na
wanachuowenzangu, na wale wote waliokuwa pamoja nasi katika shughulina
mijadala yetu.Tumepanga mhadhara huu mapema kidogo kwa sababu
mbili.Moja, wanafunzi, vijana wa Kigoda, wanaondoka leo kwendakwenye
likizo yao. Ya nini kutoa mhadhara wakati wenyewehawapo? Pili, mapema
mwezi ujao, pamoja na wasomi wenzangu
wawili, tumejipangia kwenda nje ya nchi kufanya utafiti wa
kuandika
wasifu (biography) wa Mwalimu. Kwa hivyo, tukaonatarehe ya leo ni
mwafaka.Nimegawa mhadhara huu katika sehemu kuu nne. Hoja yanguambayo
itaeleza udhani (hypothesis) wangu ulioniongozakuchambua Rasimu ni
sehemu ya kwanza. Sehemu ya piliitazumgumzia dhana ya ‘ukuu wa katiba’
ya shirikisho, yaani
supremacy of the federal constitution
.
Kwa kirefu kidogo, ‘moyo’wa rasimu, yaani muundo na taasisi za
muungano, nitazichambuakatika sehemu ya tatu. Sehemu ya mwisho, ambayo
ni ya nne,kabla sijahitimisha mhadhara wangu, itakuwa juu ya matumainiya
wananchi ya Tanzania Mpya.
Bonyeza Read More Kuendelea
HOJA
Awali ya
yote ningependa kuweka wazi, mosi, mtazamo wanguutakaoniongoza katika
kuchambua Rasimu ya Katiba Mpya; pili,jambo ambalo ninaliona kuwa ni
‘moyo wa Katiba,’ na tatu udhani(au hypothesis) wangu.
Mtazamo
Kwanza, kwa
wananchi walio wengi, mchakato wa Katiba mpyaulitoa matumaini ya mwanzo
wa kujenga Tanzania Mpya: nchina jamii zitakazojikita kwenye kujali
wavuja jasho, zenye msingiwa haki ya kijamii (social justice), na sio tu
haki ya kisheria (legaljustice). Tulitarajia kwamba tutatafakari kwa
makini hali halisiya watu wetu kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita
ambacho
kimetufikisha kwenye hali hii ya leo. Tulifikiri tutatafuta njia
mbadala
itakayorudisha imani na matumaini ya watu katikamifumo yetu ya utawala,
siasa na uchumi - mfumo unaowekamazingira na nafasi pana kwa wananchi
walio wengi kuendelezamapambano yao ya kujikomboa.Kwa dhati kabisa,
tungechagua njia mbadala itakayojengamshikamano palipo na utengano;
itakayotuelekeza kwenye usawa,palipo na mpasuko wa kitabaka, itakayo
imarisha Muunganokwa mtazamo wa Umajumui wa Afrika, palipo na mwelekeowa
kurubuni wananchi na kugawanya madaraka. Na tulitarajiakwamba Katiba
Mpya itatangaza rasmi matumaini haya nadhamira hii bila kupinda dhana au
kutafuna maneno.Haya ndio yalikuwa matumaini yetu ya Katiba Mpya na
haya ndioyatakayoniongoza katika kuchambua Rasimu. Ila nitatumia
piautaalaam wangu wa kisheria, nilioupata kutokana na wananchiwenyewe
waliogharimia elimu yangu. Huu ndio mchango wangumdogo kwa jamii
iliyonilea.
7
‘Moyo wa Katiba’
Pili, moja
kwa moja, niseme kwamba moyo wa katiba yetu, aumchakato wowote wa kuwa
na katiba mpya, ni Muungano. Hililinatokana na hali halisi ya kihistoria
ya katiba zetu. Suala laMuungano ndilo limesheheni mambo muhimu ya
mfumo wakidemokrasia na jamii. Kwa hivyo, muundo wa Muungano siosuala la
idadi ya serikali – moja, mbili, tatu, mbili na nusu n.k. –bali ni
suala la demokrasia.Isitoshe, maoni yaliyokuwa yanakusanywa yalikuwa juu
ya Katibaya Muungano, wala sio katiba ya Tanganyika au katiba ya
Zanzibar.Na Rasimu iliyokabidhibiwa kwetu kwa ajili ya kujadiliwa pia
niRasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa
hivyo,uchambuzi wangu, kwa sehemu kubwa, ni kuhusu Muungano.
Udhani (hypothesis)
Baada ya
kuisoma Rasimu kwa kina, mimi nadhani kwambamasharti mengi ya Rasimu na
muundo wake mzima ni matokeo yamivutano mikali katika Tume. Bahati mbaya
hatuna mwenendo wamajadiliano ya Tume wala taarifa yao rasmi, hata
taarifa ya awali.Lakini usomaji wangu wa awali unaniambia kwamba Rasimu
hiini maelewano kwa maana ya
compromise, na sio mapatano, aumwafaka, kwa maana ya consensus. Nijieleze kidogo.Katika maelewano au compromise,
pande zinazokinzana hatimayezinakubali kwa shingo upande ili
kutokukwamisha maamuzi.Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na
kila upandehuwa na mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili.
Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi kuwa kwa moyo safi.
Maelewano au
compromise, yanazaa uamuzi legelege.Mapatano au consensus, kwa upande mwingine, ni maafikianoyanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila mmoja akilenga
kuthibitisha hoja yake na kwa njia hii kusadikisha wenzake
8
kwamba hoja yake ni sahihi. Baada ya kufikia uamuzi wa mwafaka,
kila mmoja anatoka akiwa ameridhika na amefurahi. Katika
compromise
, kila mmoja anatoka amenuna. Ni wazi kwambahuwezi ukapata mwafaka fastafasta.
Lazima utachukua muda.Ili nieleweke vizuri, nitoe mifano miwili, mmoja
mwepesi,mwingine mzito. Ib. 1(3) ya Rasimu inasema:Hati ya Makubaliano
ya Muungano iliyorejewa katikaIbara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa
Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa
kadriitakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo waMakubaliano hayo.Maana
ya aya hii ni:Hati ya Makubaliano ya 1964 ni msingi wa Katiba hii
(yaaniRasimu); naKatiba hii ni mwendelezo wa Makubaliano.Ukiangalia kwa
jicho la kisheria, , ukisema Hati ndio msingi, maanayake ni kwamba Hati
bado inaendelea kuwa na nguvu ya kisheriana ndio sheria kuu inayotawala
Katiba. Lakini Hati iliweka serikalimbili; sasa, iweje rasimu
inayozungumzia serikali tatu iwe namsingi ambao ulijengeka kwenye
serikali mbili?La pili, Katiba iliyojikita kwenye serikali tatu haiwezi,
kwa vyovyotevile, ikawa mwendelezo wa Hati.Ni kweli kabisa kwamba Hati
ya Makubaliano ya 1964 ni chanzocha Muungano. Historia hii, kama
inavyostahili, imewekwa kwenyeUtangulizi. Lakini masharti ya katiba
yenye nguvu za kisheriahayawezi tena kurudia historia. Ukitaja maneno
kama haya katikamasharti ya Katiba, kimahakama inachukuliwa kwamba nia
yakoilikuwa kuipa Hati nguvu ya kisheria. Nina uhakika kabisa
kwambahaikuwa nia ya Tume kuifufua Hati ya 1964 na kuipa nguvu
yakisheria.
9
Pia,
ninaamini kabisa kwamba Tume iliyosheheni wanasheriawazoefu na
waliobobea huenda walijua na kuelewa kabisawalichokuwa wanaandika. Kwa
hivyo, haiwezekani kwambawalikosea, au kuteleza, bali ilikuwa ‘kusalimu
amri’ na “kuelewana”ili mambo yaendelee. Ndivyo tulivyopata ibara
legalege ambayokisheria haina kichwa wala mkia.Inawezekana kabisa kwamba
ibara hii isiwe na madhara makubwakwa sababu majaji wenye busara, kwa
hakika, hawatatia maananisharti kama hili. Lakini unaweza kupata jaji
ambaye anaegemeazaidi kwenye ufundi na kuitafsiri ibara hii kama ilivyo.
Madharayake yanaweza kuwa makubwa. Vyovyote vile, ibara kama
hiiisiyoeleweka inashusha hadhi ya Katiba.Mfano wa pili, mzito zaidi, ni
kuhusu mipaka ya madaraka. Eneola utawala wa Serikali ya Shirikisho
limetajwa kuwa ‘eneo lote laTanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya
bahari na eneo lotela Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari’ (ib.
2). Lakinieneo la utawala wa serikali ya Bara na serikali ya
Zanzibarhalikutajwa. Bila shaka, katiba za Washirika zitataja maeneo
yaona kuna uwezekano mkubwa kwamba kutakuwa na msuguanona kutoelewana
hasa juu ya mipaka ya bahari katika ‘Zanzibarchannel’. Katiba ya
Zanzibar ya Mwaka wa 1984 iliopo, kwa mfano,inataja mipaka ya Zanzibar
kuwa ni ‘eneo lote la Visiwa vya Ungujana Pemba pamoja na Visiwa vidogo
vilivyoizunguka na bahari yakeambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwaJamhuri ya Watu wa Zanzibar.’ (ib.1)Pande mbili za
Muungano zimewahi kutofautiana kuhusu eneolao la bahari, hasa kwa sababu
inadhaniwa kwamba bahariinayopakana na maeneo ya Tanganyika na Zanzibar
ina mafuta narasilimali nyingine. Waziri Tibaijuka alipopeleka ombi
Umoja waMataifa kuongeza eneo la nchi kwa maili 150, mjumbe mmoja
waBaraza la Wawakilishi aliwasilisha hoja binafsi kumlaumu Waziri
10
wa Zanzibar mhusika kwa kuridhia ombi hilo.
1
Ukimya wa
Rasimu juu ya kueleza kwa uwazi mipaka ya utawalawa Washirika ni wa
ajabu kweli kwa sababu ni wazi kwambahuwezi kuzungumzia utawala wa
mamlaka yoyote yale bilakubaini mipaka yake. Ukimya huu unaweza kuzaa
migogoro.Nitaendelea kutoa mifano mingine katika uchambuzi
wanguunaofuata.
***
Sasa, ni juu
yangu kuthibitisha udhani (au hypothesis) wangu.Kabla sijaanza kufanya
hivyo, ningependa kusema kwa dhatikabisa kwamba Tume hii ya watu 32
wenye kuwakilisha maslahitofauti na hisia mbalimbali ilifanya kazi
katika mazingira na halingumu sana. Hayo yalitegemewa kutokana na mfumo
wenyewe waTume. Wachache wetu tulitahadharisha mapema lakini
viongoziwaliosheheni busara wakaamua vinginevyo.Katika hali hii,
mhadhara wangu usichukuliwe hata kidogo kamakuibeza au kuipuuza kazi
waliyofanya akina Mzee Warioba nawenzake. Sina shaka kwamba wengine wao
walipoteza usingizina hata kuteseka moyoni mwao kuhusu maaumuzi
menginewaliyoyafanya. Kwa hili, wanastahili pole zetu, zaidi ya pongezi.
II.
UKUU WA KATIBA(SUPREMACY OF THE CONSTITUTION)
Magwiji wa
katiba (Wheare 1966, Singh 1994: A-29 na kuendelea,Nwabueze 2003: juz.
1, sura 3, Seervai 1997: juz. 1, sura v, Shivji
1990/2009) wanaafiki kwamba mfumo wa shirikisho una angalau
sifa ku nne. Hizo ni:
11
Kwamba
mwananchi anatawaliwa na serikali mbili, yaani serikaliya shirikisho na
serikali ya mshirika;Kwamba kuna mgawanyo wa madaraka miongoni mwa
serikali;Kwamba Washirika, na katiba na sheria zao, zina hadhi sawa;
naKwamba Katiba ya Shirikisho ni sheria kuu (supreme law).Je, Rasimu
inakidhi sifa hizi? Kwa maoni yangu, kwa kiasi kikubwa,mfumo wa
shirikisho katika Rasimu unakidhi sifa tatu za awali.Kila mwananchi
pande zote mbili atatawaliwa na serikali mbili;Wabara watatawaliwa na
Serikali ya Shirikisho na Serikali ya Bara,Wazanzibari watatawaliwa na
Serikali ya Shirikisho na serikali yaZanzibar. Pia kuna mgawanyo wa
madaraka kati ya serikali tatu.Washirika, yaani Bara na Zanzibar wana
hadhi sawa (ib. 61(5)).Sifa inayotatanisha ni ya mwisho, ile inayosema
kwamba Katibaya Shirikisho ni sheria kuu. Nitazichambua ibara
zinazohusika.Kabla sijafanya hivyo, nieleze kwa muhtasari tu maana na
dhanaya Ukuu wa Katiba (supremacy of the constitution).‘Ukuu wa Katiba’
maana yake ni sheria zote, madaraka, majukumuna mamlaka yanatokana na
katiba na katiba ndio chanzo chauhalali wa utawala. Katiba yenyewe
inapata mamlaka yake kutokakwa wananchi katika ujumla wao. Ndiyo maana,
katika msamiatiwa kawaida, tunasema katiba ni sheria mama. Nikitumia
msamiatihuo kwa katiba ya shirikisho, naweza nikasema kwamba katibaya
shirikisho ndio mama na baba wa shirikisho. Katiba na sheriaza
Washirika, ingawa zina mamlaka kamili katika maeneo yao,zinatokana na
katiba ya shirikisho na zinapata uhai wao wa kisheriakwa mujibu wa
katiba ya shirikisho. Muhimu zaidi ni kwamba,kama kuna masharti ya
katiba au sheria za Washirika ambazozinakinzana na katiba au sheria za
shirikisho zilizopitishwa kwamujibu wa katiba ya shirikisho, basi sharti
husika inakuwa batilikwa kiasi kile. Kwa lugha ya kimombo dhana hii
inaitwa
supremacy
12
clause,
yaani
kipengele cha ukuu wa katiba ya shirikisho. Katikakatiba zote za
shirikisho duniani kuna kipengele cha ukuu;Marekani, Australia, India,
Canada n.k. Sitazinukuu zote isipokuwambili, Katiba za Marekani na
Australia. Ibara ya VI ya Katiba yaMarekani inasema:
This
Constitution, and the Laws of the United States whichshall be made in
Pursuance thereof; and all Treaties made,or which shall be made, under
the Authority of the UnitedStates, shall be the supreme Law of the Land;
and theJudges in every State shall be bound thereby, any Thingin the
Constitution or Laws of any State to the Contrarynotwithstanding.
Na kifungu
109 cha Katiba ya Australia kinasema hivi:When a law of a State is
inconsistent with a law of theCommonwealth, the latter shall prevail,
and the formershall, to the extent of the inconsistency, be invalid.Kwa
kifupi, vipengele vyote viwili vinasisitiza ukuu wa katibaya shirikisho.
Na hii ina mantiki na umuhimu wake usiopingika.Ukitaka shirikisho liwe
imara na liwe na nguvu, basi hakunabudi Washirika wakubali kutambua na
kutii masharti ya katibaya shirikisho. Bila hivyo, shirikisho litayumba
na kutakuwa namigogoro kutokana na vipengele vya katiba na sheria na
vitendovya vyombo vya Washirika kukinzana na kugongana kila mara.Sasa
tuangalie vipengele vya Rasimu vinasemaje kuhusu ukuu waKatiba ya
Shirikisho. Ibara 8(1) inasema:Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za
Washirika waMuungano kwa mambo
yasiyo ya Muungano, Katibahii itakuwa sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano.(Msisitizo wangu)
13
Hii ina
maana kwamba ukuu wa Katiba ya Shirikisho ni kwamambo saba tu ya
muungano yaliyotajwa katika nyongeza; lichaya mambo hayo, katiba za
Washirika ni sheria kuu katika maeneoyao kwa mambo yote mengine
yaliyosalia (
residual powers).Tuendelee.
Ibara ya 61(4) inasema:Washirika wa muungano watatekeleza majukumu
yaokwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.‘Kuzingatia’ sio
kubanwa; Kiingereza chake ni ‘to take accountof’, ‘to bear in mind’.
Unaweza ukazingatia masharti ya Katibaya Shirikisho na baada ya hapo
ukatenda kinyume chake, lakinihata hivyo utakuwa hujavunja katiba. Hii
inaeleweka zaidiukisoma ibara ndogo inayofuata inayotaka Washirika
kutekelezamajukumu yao kwa masuala yasiyo ya Muungano ‘kwa mujibu’wamasharti ya katiba zao. ‘Kwa mujibu’ inaleta maana ya kubanwa,huwezi ukakiuka. Kwa hivyo, masharti ya Katiba ya Shirikisho
yanakushawishi
; masharti ya katiba ya Mshirika yanakushurutisha.Niangalie
ibara nyingine ya mwisho ambayo inakaribia kidogokuuzungumzia ukuu wa
Katiba ya Shirikisho. Ibara 109(5)inasema:Bila ya kuathiri kutumika kwa
Katiba ya Tanzania Barana Katiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na
nguvuya sheria katika Jamhuri ya Muungano kwa mamboyanayohusu Muungano
na endapo sheria nyingineyoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba
hii,basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiukaKatiba hii,
itakuwa batili.Kuna dhana mbili zilizotumika katika kipengele hiki:
‘mamboyanayohusu’ (Muungano) na ‘sheria’. Bila shaka ‘mamboyanayohusu
Muungano’ ni dhana pana zaidi kuliko ‘mambo ya
14
Muungano’.
Mambo ya Muungano ni yale saba yaliyotajwa katikanyongeza. Mambo
yanayohusu Muungano ni hayo saba pamojana yale yote yaliyozungumziwa
katika Katiba ya Shirikisho. Kwamantiki hiyo hiyo, neno ‘sheria’
haliwezi likawa na maana panazaidi ya sheria inayohusu mambo ya Muungano
yanayotungwa naBunge la Shirikisho kwa mujibu wa ibara 109. Kwa hivyo,
ukuu waKatiba ya Shirikisho unaozungumziwa katika ibara hii ni juu
yashughuli za Muungano tu. Sheria yoyote juu ya mambo yanayohusuMuungano
ikikiuka masharti ya Katiba ya Shirikisho, sheria hiyoni batili. Lakini
hii haihusu katiba na sheria za Washirika.Uchambuzi wangu wa ibara hizi
zote zinazohusu hadhi ya Katiba yaShirikisho katika uhusiano wake na
katiba na sheria za Washirika,unaweza kuhitimishwa kama ifuatavyo:Mosi,
hakuna popote pale katika Rasimu tunapokuta Ukuu waKatiba ya Shirikisho
(kwa maana ya
supremacy clause)
umewekwakwa uwazi na ufasaha, kama ilivyo katika katiba nyingine
zashirikisho nilizozitaja hapo awali.Pili, vipengele vinavyohusika, ama
vinatatanisha au viko kimya, auyote mawili, kuhusu kipengele cha
ukuu.Tatu, hii, kwa maoni yangu, haikutokea kwa makosa au kwakuteleza
bali ni tokeo la maelewano kwa maana ya compromise.Nathubutu
kusema kwamba kama jambo hili lingejadiliwa katikaTume, kungekuwa na
mvutano mkali sana.Mwisho, utatanishi na ukimya huu utapalilia vyanzo
vya migogorona mivutano kati ya mamlaka ya Washirika na Muungano siku
zausoni. Athari zake haziwezi kuepukika. Nitatoa mifano michachemuhimu
kadri ninavyoendelea na mhadhara wangu.
15
A.Tunu, Dira, na Malengo
Rasimu ina
Tunu, Dira na Malengo ambayo yamesistizwa sanana Mwenyekiti wa Tume,
Mheshimiwa Mzee Warioba. Yaliyomokatika Tunu, Dira, na Malengo ni udugu,
utu, umoja, uzalendo,uwazi, n.k. na haya yamerudiwarudiwa. Kwa upande
wangu,sitasemea hayo. Kwa kadri nijuavyo, hakuna utawala popote
paleduniani, uwe wa kibepari, kijamaa au wa mabavu, utakaopingahizi
Tunu, hata kama hawatekelezi. Lakini jambo mojawapoambalo liko kwenye
utangulizi (ib. 1(2)) na Malengo (ib. 11(1)) nisuala zima la
kujitegemea. Kwa mfano, lengo kuu mojawapo katikaMalengo (ib. 11(1))
linasema na ninanukuu:Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha
nakudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wawananchi wa Jamhuri ya
Muungano kwa kuzingatiaustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru
lenyedemokrasia, utawala bora na
kujitegemea (msisitizowangu).Nimechagua
ibara hii kuizungumzia kwa sababu kujitegemeakuna nafasi ya kipekee
katika historia yetu ya kisiasa. Mwalimuna Sokoine walikuwa wanasistiza
sana umuhimu wa kujitegemeakwa hoja kwamba tusipojitegemea tutapoteza
uhuru wetu.Pamoja na hili, kwetu sisi mtazamo wa kujitegemea uliendanana
ujamaa, ujamaa na kujitegemea.
Haya mawili yalikuwa kamachanda na pete. Sasa ujamaa umefutwa kabisa
katika Rasimu kwahoja kwamba ni itikadi (kana kwamba soko huria,
ubinafsishajin.k. sio itikadi). Kwa vyovyote vile, kidole kimekatwa,
tumebakina pete inahengihengi.Niendelee na mfano wangu. Sura ya Pili
inazungumzia MalengoMuhimu. Malengo yapo katika Katiba ya sasa lakini
Malengoyalivyowekwa katika Rasimu, yanaturudisha nyuma hatua mbili.
16
Kwa nini?
Kwanza, katika Rasimu Malengo ni mwongozo kwahivyo hayabani kisheria.
Katika Katiba iliopo Malengo yana nguvuya sheria (ib. 7(1)) ingawa sio
kimahakama (ib 7(2)). Pili Malengokatika Rasimu ni kwa ajili ya vyombo
vya Muungano tu (ang. ib.10(1) na ib. 238(1) maana ya neno ‘serikali’).
Katika katiba iliopoMalengo yalibana vyombo vyote vya serikali zote
mbili.Lakini hata kama yangekuwa yanabana vyombo vya Washirika,bado
yasingekuwa na nguvu ya sheria kwao. Hii ni kwa sababuya kutokuwa na
kipengele cha ukuu. Kwa mfano, inaweza kutokeawashauri waelekezi wa
ndani na nje wakaishauri serikali yaTanganyika
2 kwamba
mtazamo wa kujitegemea umepitwa nawakati katika dunia ya utandawazi.
Katika utandawazi kunakutegemeana, sio kujitegemea. Isitoshe, washauri
wataendelea,tukiweka mtazamo wa kujitegemea, ambao unahusishwa naujamaa,
katika katiba, kuna hatari ya kutoweza kuvutia uwekezajikutoka nje.
Kutokana na ushauri huo, katika katiba ya Tanganyika,lengo kuu linaweza
likasomeka hivi:
Lengo kuu la
Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu,amani, umoja na
utengamano wa wananchi wa Tanganyika kwakuzingatia ustawi wa wananchi na
kujenga Tanganyika huru yenyedemokrasia, utandawazi bora na
kutegemeana.
Pasipo na
shaka, lengo hili linagongana na lengo kuu la Katiba yaShirikisho. Hata
hivyo, ndio lengo litakalo ongoza vyombo vyaTanganyika kwa sababu Katiba
ya Shirikisho haiko juu ya katibaza Washirika; yaani, inakosa ukuu.Kwa
mujibu wa lengo jingine (ib. 11(1)(xi), Serikali inaagizwa‘kuweka
utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezajiwa haki ya mtu
kujipatia elimu …’. Serikali inayomaanishwakatika kipengele hicho ni
Serikali ya Muungano, lakini Serikaliya Muungano haisimamii elimu kwa
sababu elimu sio jambo la
17
Muungano. Na
inawezekana kabisa katiba za Washirika zisiwe nalengo linalofanana na
hili. Kwa hivyo, lengo hili jema halina maana- chombo kinachoagizwa
kutekeleza lengo, hakisimamii elimu,na vyombo vya Washirika
vinavyosimamia elimu havibanwi nalengo. Kwa hivyo, jambo linalopendeza
kulisikia ni ganda tupu bilatunda!Kwa hitimisho, nigusie ibara (10)(2)
ambayo inaagiza Serikali yaMuungano kutoa taarifa Bungeni juu ya
utekelezaji wa Malengoangalau mara moja kwa mwaka. Swali ni kwamba
malengo yotemuhimu yanaangukia chini ya mamlaka ya Washirika ambaoni
watekelezaji na hawabanwi na Katiba ya Shirikisho. Katikaukweli huu, hii
taarifa itakayowasilishwa Bungeni itakuwa na ninina itakuwa na maana
gani. Kwa kifupi basi, watekelezaji wakuuwa Malengo hawabanwi na
masharti haya; yule ambaye siomtekelezaji ndiye anayebanwa!
B. Maadili na Miiko ya Uongozi
Mzee Warioba
pia amechangamkia maadili na miiko ya viongoziiliyowekwa katika Rasimu,
Sura ya Tatu. Kuna ibara kama nanepamoja na ibara ndogo chungu nzima
juu ya suala la maadili namiiko. Hizi zinawahusu viongozi wa kuchaguliwa
na kuteuliwana ambao watatajwa katika sheria ya Bunge (ib.14(3)).
Bungelinalozungumziwa hapa ni Bunge la Muungano. Lakini Katiba
zaWashirika hazihitaji kufuata au kuwa sambamba na vipengelehivyo. Wana
hiari kuweka au kutokuweka, au kurekebisha aukuchagua vipengele
wanavyotaka kwa sababu maadili na miiko siojambo la muungano na Katiba
ya Shirikisho haiwabani Washirika.Kwa mfano, ib.20(2)(a)(iii) inasema
kwamba kiongozi wa ummahapaswi ‘kujilimbikizia mali kinyume na sheria’.
Sasa, sheria ipiinayozungumziwa hapa? Je kama hakuna sheria ya
Washirikainayokataza viongozi wa umma kujilimbikizia mali, kipengele
18
hiki katika
Katiba ya Shirikisho kitakuwa na uzito gani? Ni wazi,haiwezi ikawa na
nguvu yoyote katika maeneo ya Washirika.Sasa nimulike kwenye haki za
binadamu.
C. Haki za Binadamu
Wakereketwa
wameshangilia sana haki za binadamu katikaRasimu na wana sababu nzuri tu
kufanya hivyo. Rasimu imeelezakwa ufasaha haki za binadamu na imeongeza
haki nyingineambazo hazimo katika katiba zilizopo. Kuna mapungufu hapa
napale lakini haya yanarekebishika. Kwa mfano, haki ya
wananachikuandamana kuonyesha hisia zao za kulaumu au kutoridhika
najambo fulani haikuwekwa. Pia hakuna haki ya wafanyakazi kugomakama
silaha yao muhimu ya kushinikiza waajiri wao kutekelezamatakwa yao.Kuna
haki mbili muhimu ningependa kuzitaja hapa. Ib. 39(3)inaeleza kwamba
raia wa Jamhuri ya Muungano ‘hatapelekwakatika nchi ya nje yoyote kujibu
mashtaka au kufanyiwa mahojianoya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.’
Hili ni jambo jema;hususan inapiga marufuku ile inayoitwa ‘rendition’.
3 Pendekezolangu
ni kuongeza vipengele viwili kuweka wazi kwamba nimarufuku raia wa
Jamhuri (a) ‘kufungwa au kuwekwa kizuizininchi ya nje bila ya kufuata
sheria ya nchi hiyo; na (b) ‘kuhojiwa
na maafisa wa ujasusi au usalama wa nchi za nje katika eneo la
Jamhuri’.
4
Lakini suala
ambalo linatatanisha ni: Hati hii nzuri ya haki zabinadamu ina uzito
gani katika maeneo ya Washirika? Haki zabinadamu sio jambo la Muungano
na Katiba ya Shirikisho sio Katibamama. Je, kama katiba za Washirika
zikikosa vipengele vinginevya haki au kuandikwa tofauti na kuwa na maana
na tafsiri tofauti,itakuwaje?
5 Nitoe mfano. Katika kutekeleza haki ya mwananchikushiriki katika utawala, wagombea huru wanaruhusiwa na
19
Rasimu
katika ngazi zote za utawala. Iwapo katiba za Washirikahazina kipengele
kama hicho, basi mgombea huru atakuwa nahaki ya kugombea uchaguzi katika
ngazi ya Bunge la Muunganona Urais wa Muungano tu, lakini hakuna
mgombea huru atakuwana haki kugombea nafasi za serikali za mitaa au
mabunge yaWashirika au urais wa Tanganyika au Zanzibar.
6 Huu ni mfanomwingine wa wananchi kupewa ganda bila tunda.
Sasa nimefikia sehemu muhimu ya mhadhara wangu, muundo na
taasisi za muungano.
III.
MUUNDO NA TAASISI ZA SHIRIKISHO
Hitimisho
langu juu ya muundo wa muungano ni kwamba, mosi, nitegemezi na, pili, ni
dhaifu kwa sababu umejengwa juu ya msingiwa mchanga wa dhamira na nia
nzuri badala ya msingi wa maweya nguvu za kikatiba zilizowekwa na
wananchi wenyewe. Ni kamakwamba suala la Muungano ni ujirani mwema
badala ya umojawa nchi. Nitalifafanua kwa kuchambua mifano ya maeneo
kamamanane hivi.
A.Taasisi Kuu za Kusimamia Muungano
Muungano wa
Jamhuri ya Muungano umeainishwa kama shirikisholenye serikali tatu (ib.
57(1), serikali ya muungano au shirikisho,serikali ya Tanzania Bara na
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7
Kwa maoni
yangu, kwa usahihi zaidi, hizi zingeitwa dola tatu kwasababu zote zina
mihimili mitatu ya dola, yaani, serikali, bunge namahakama, na mamlaka
yao ya utawala. Kwa kukwepa kuainishana kutaja kwa jina lake dhana
inayokusudiwa, ina athari zakeza kutokuelewana na kuzaa mizozo isiokuwa
ya lazima. Mfanomzuri ni yale malumbano yaliyotokea juu ya Zanzibar kuwa
nchiau sio nchi.
8 Inawezekana, kwa busara zake, Tume ilichagua kwa
20
maksudi
msamiati uliozoeleka kuepuka malumbano juu ya maanaya dola na nchi.
Tuachane na hili, tuendelee.Kuna taasisi mbili za mahusiano baina ya
serikali hizi tatu -, Tumeya Uhusiano na Uratibu wa Serikali (ib.102(1)
na Mawaziri Wakaazi(ib. 64). Mawaziri Wakaazi watateuliwa na Washirika
na watakuwa
na ofisi zao Makao Makuu ya Serikali ya Muungano. Eneo la Makao
Makuu
halijulikani kama litakuwa katika eneo la Tanganyikaau Zanzibar, au
litakuwa linahamahama kati ya Tanganyika naZanzibar. Vyovyote vile,
itabidi serikali ya muungano iombe
serikali za Washirika kuipatia eneo lake la kujenga ofisi za makao
makuu pamoja na Ikulu ya Rais wa Muungano.
9 Jukumu
mahsusila hao Mawaziri Wakaazi ni kusimamia uhusiano baina ya
serikaliza Washirika, kwa upande mmoja, na kati ya Serikali ya
Muunganona serikali ya Mshirika mhusika, kwa upande mwingine.Tume ya
Uhusiano ina wajumbe sita - makamu wa rais waMuungano, ambaye atakuwa
mwenyekiti, marais wawili waWashirika, Mawaziri wawili Wakaazi na waziri
mwenye dhamanaya mambo ya nje ya Muungano (ib. 102(2). Jukumu na lengo
kuula Tume ni kusimamia na kuweka taratibu na mazingira mazuriya
mashauriano, mashirikiano, na utatuzi wa migogoro baina yaserikali tatu
(ib. 103-104). Kwa jumla, Tume ya Uhusiano siochombo cha utendaji
(executive) isipokuwa tu kitahusika katikautatuzi wa migogoro ambao
nitauzungumzia hivi punde. Katikahali halisi ya ulinganisho wa nguvu za
kisiasa, sidhani kwambaTume inaweza kufanya maamuzi yanayobana pande
zote husika,
bali, zaidi ni kufikia maelewano, ambayo pia huwezi kuwa na
hakika kwamba yatatekelezwa. Isitoshe, marais hawa watatuwakitoka vyama tofauti (mbali na wagombea binafsi), vyenye sera
na mielekeo tofauti, hata kufikia maelewano inaweza kushindikana
na kusababisha mivutano na migogro isiyokuwa na mwisho.Pili, katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro, tume inaweza
21
kufanya
uamuzi lakini upande wowote ambao haukuridhika unahaki ya kukata rufani
katika Mahakama ya Juu na uamuzi waMahakama unakuwa wa mwisho (ib.
104(1)(e) Kwa vyovyote vile,Tume sio ngazi ya kwanza katika kutatua
mgogoro kwa sababupande zote hazilazimishwi kuanzia mgogoro katika Tume
bali zinahiari ya kuanzia ama katika Tume au katika Mahakama.Kwa
kujumuisha, navyoona mie, chombo hiki kikuu cha kiungobaina ya serikali
tatu, kitakuwa na changamoto kama tatu hiviambazo zinaweza zikageuka
kuwa matatizo.Mosi, kuna suala la protokali. Marais kuwa chini ya
uenyekitiwa Makamu wa Rais ina utata. Katika hali ya kawaida, masualaya
protokali yasingekuwa ya kuzingatiwa lakini kwa sababuzisizoeleweka
wakuu wa nchi zetu wanajali sana protokali, labdakudhihirisha ukuu
wao.Pili, ambayo ni muhimu zaidi, hakuna uwiano wa nguvu za
kisiasakatika Tume. Kwa vyovyote vile, mwenye nguvu katika Tumeatakuwa
Rais wa Bara - yeye ndiye mtawala wa eneo kubwalenye wananchi wengi,
yeye ndio mwenye rasilimali nyingi,yeye ndiye anatoa mchango mkubwa wa
kuendesha serikali yamuungano, ikiwemo gharama za Tume yenyewe. Kwa
hivyo,tupende tusipende, yeye ndiye atakuwa na sauti nzito.
Isitoshe,kutokana na muundo wa serikali tatu, rais wa Bara hataona
aibukujitutumua kinyume na ilivyo katika serikali mbili wakati
raismwenye dhamana ya Bara pia ni rais wa muungano.Tatu, ikiwa Tume
inataka kufanya uamuzi wowote, itakuwa vigumukwa sababu kila upande
unawakilishwa na watu wawili wawili.Nne, katika hali hiyo, mara nyingi,
hasa katika masuala nyeti au
mazito ya kitaifa, hata kufikia maelewano itakuwa vigumu. Kati ya
Washirika, unaweza kukuta kila mara upande dhaifu ambao hojazake zinaelekea kutokubalika, ataomba kikao kiahirishwe ili arudi
22
kwake kushauriana na wenzake au kupata maoni ya wananchiwake. Kwa wanasiasa, hii inakuwa ni mbinu ya kuahirisha
maafikiano, yaani,
delaying tactics.Kwa
jumla, na bila kubeza, tathmini yangu ya Tume hii ni kwambahaina
tofauti ya msingi na zile kamati zisizoisha za akina Shekilangojuu ya
kero za Muungano.
B. Bunge la Muungano
Mamlaka ya
kutunga sheria juu ya mambo yote yanayohusuMuungano yamewekwa chini ya
Bunge la Muungano. Mambo ‘yoteyasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge
la Tanzania Barana Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.’ Bila shaka,
mamlaka hayayatatumika kwa mujibu wa Katiba zao. Kuhusu Bunge,
nitagusiamambo matatu yanayotatiza.Moja, ni majimbo ya uchaguzi wa Bunge
la Muungano. Kwamujibu wa ib. 105(3) ‘kila mkoa kwa upande wa Tanzania
Barana wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la
uchaguzi’.Wanahabari wetu waliobobea wamekwishapiga hesabu. Kunamikoa 25
Bara na wilaya 10 Zanzibar. Kwa kuwa watakuwepowabunge wawili kutoka
kila jimbo, mmoja wa kiume na mwinginewa kike (ib. 104(4), basi tutakuwa
na wabunge 70, 50 kutokaBara na 20 kutoka Zanzibar. Pia watakuwepo
wabunge watanokuwakilisha kundi la walemavu ambao watateuliwa na Rais
wamuungano. Naona tunaweza kutabiri kwamba watatu watatokaBara na wawili
watatoka Zanzibar ili kuwe na uwiano na idadiya watu. Jumla tutakuwa na
wabunge wa Bara 53, ambayo niasilimia 71, na 22 kutoka Zanzibar, ambayo
ni asilimia 29. Kwahivyo, uwiano wa Bara na Zanzibar ni asilimia 71 kwa
asilimia 29,Wabara wakiwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote.
Uwianohuu moja kwa moja unapingana na msingi wa kwanza kabisawa
shirikisho. Shirikisho linasimama kwenye usawa wa kisiasa
23
(
political equality)
wa Washirika bila kujali ukubwa au idadi yawatu wao. Kwa hivyo,
uwakilishi wao hasa katika chombo chakutunga sheria unatakiwa kuwa
sawa.Lakini kuna jambo jingine la kutatanisha. Mikoa na wilaya ningazi
za utawala ambazo haziko chini ya mamlaka ya Muungano.Ugawaji wa maeneo
ya utawala ni mamlaka ya vyombo vyaWashirika, hususan Rais. Kwa mfano,
kwa mujibu wa ibara 2Aya Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais ndiye mwenye
mamlaka yakugawa maeneo ya mikoa na wilaya. Sioni sababu ya
Zanzibarkukibadilisha kipengele hiki kwa sababu hawashurutishwi naKatiba
ya Shirikisho (Rasimu) kufanya hivyo. Isitoshe, hakunachochote katika
Rasimu kumzuia rais au marais wa Washirikakubadilisha mipaka na kuongeza
idadi ya mikoa au wilaya katikamaeneo yao.Tuchukue mfano. Kwa sababu
zozote zile, rais wa Zanzibaranaamua kugawa Zanzibar katika wilaya 20.
Hii itamaanishakwamba kutakuwa na wabunge 40 kutoka Zanzibar, ikifanya
jumlaya wabunge kuwa 95 badala ya 75 katika Bunge. Mabadiliko hayamara
moja yatakuwa yamebadili uwiano kati ya Bara na Zanzibar- asilimia 56
kutoka Bara na 44 kutoka Zanzibar. Na, je, jambohili likitokea katikati
ya muda wa Bunge, kutakuwa na uchaguzimpya? Nimesema rais anaweza
kufanya hivyo kwa sababu zozotezile lakini pia anaweza kufanya hivyo kwa
maksudi ili kujiongezeauwakilishi katika Bunge la Muungano. Kwa lugha
ya kimombo, hiiinaitwa gerrymandering.
Vilevile, kwa upande wa Bara, rais waTanganyika anaweza kuongeza idadi
ya mikoa.Pili, Rasimu inaruhusu wagombea huru na pia uwezo wa wapigakura
kumuondoa mbunge wao hata kabla ya kipindi chake kwasababu zilizotajwa (right of recall) (ib.
124). Mambo haya yotemawili yanahusika na wabunge wa Bunge la Muungano
nasio mabunge ya Washirika. Kwa hivyo, Washirika wanaweza
24
wakaamua
bila kuvunja katiba ya Shirikisho kwamba katikamaeneo yao hawatakuwa na
wagombea huru wala haki yawapigakura kuondoa wabunge wao. Na hii sio
nadharia tu.Viongozi watarajiwa wamekwishaanza kuonyesha wasiwasi
waokuhusu mgombea huru na haki ya wananchi kuweza kumuondoambunge wao
kabla ya muda.Jambo la tatu linawagusa wananchi kwa karibu sana. Ib.
107(2)(h)inaeleza kwamba miongoni mwa madaraka ya Bunge ni ‘kujadilina
kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali na
maliasilizinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.’ Jambo
hilini jema kabisa na la kulifurahia, angalau mikataba hii
izungumzweBungeni kwa uwazi badala ya wananchi kuambiwa kwamba nisiri ya
kibiashara. Lakini, rasilimali na maliasili – ardhi, mafuta,madini,
gesiasilia, maji, mapori, n.k. – sio jambo la Muungano.Rasilimali na
maliasili ni chini ya mamlaka ya Washirika nawao ndio watayasimamia.
Katika hali hii, Serikali ya Muunganoitaingia kwenye mikataba ipi na
kuhusu rasilimali gani? Ni mfanomwingine wa wananchi kulishwa maneno
matamu yasiyo nauhalisia. Ni haki hewa.Sasa niangalie taasisi nyingine
nyeti na muhimu, jeshi la polisi.
C. Jeshi la Polisi
Nianze kwa
kuweka wazi kwamba polisi haimo miongoni mwa yalemambo saba ya Muungano
kinyume na katiba ilioko (Nyongezaya Kwanza, jambo la nne). Pamoja na
kutamka kwamba Jeshi laPolisi ni chini ya mamlaka ya Muungano na jeshi
ndilo litakuwana jukumu la ‘ulinzi wa watu na mali zao’ (ib. 227(1),
Rasimuinasema kwamba ‘Washirika … wanaweza kuanzisha vikosi vyaulinzi
vitakavyosimamia masuala ya usalama wa watu na malikatika maeneo yao.’
(ib. 232(1) Bila kutafuna maneno, ibara hiini wazi na maana yake ni
kwamba Washirika wanaweza wakawa
25
na majeshi
yao ya polisi, ilimradi yasiitwe polisi kwa jina, ingawayana majukumu na
muundo unaofanana kabisa na ule wa Jeshi laPolisi. Kwa hivyo, utakuta
kuna majeshi matatu ambayo majukumuyao ni yale yale. Katika hali hii
huwezi kuepuka migongano nakama tujuavyo vikundi vyenye silaha
vikigongana, unaoathirika niusalama wa wananchi. Bila shaka, waandishi
wa Rasimu walionauwezekano huo; usuluhishi wao ni kuongeza kipengele
kinginekinachosema, ‘Vikosi vya ulinzi vya Washirika wa
Muungano,vitatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi
laJamhuri ya Muungano ili kuepusha mgongano wa mamlaka …‘ (ib. 232(2).
Tuwe wa kweli, jambo muhimu kama uwezekanowa migongano kati ya majeshi
unaweza kweli kuliachia nia nadhamira njema ya kushirikiana? Tena
kikatiba? Busara inahitajikwamba angalau kikatiba unaweka mazingira na
masharti yakuepuka migongano, sio kuweka mazingira ya migongano na
halafuukasema washirikiane ili kuepuka migongano. Haileti maana
walahaina mantiki. Ndio maana huwezi ukawa na vikosi vya usalamazaidi ya
kimoja vyenye majukumu yale yale wakifanya kazi katikamaeneo yale yale.
Kama busara ingetumika, basi ‘polisi’ ingewekakatika orodha ya mambo ya
muungano na lingeundwa jeshi mojatu la polisi la Jamhuri ya Muungano.
Na ingekuwa marufuku mtu,taasisi au serikali nyingine yoyote kuunda
vikosi vya usalamahuru nje ya jeshi la Jamhuri.Kwani wajumbe wazito wa
Tume hawakuwa na busara auhawakuliona hili? La hasha, wajumbe wengine
katika Tumewana busara tele, utaalam wa mambo ya kikatiba na tena
wanauzoefu wa kuendesha nchi kwa zaidi ya robo karne. Kwa
hivyo,ninashawishika kueleza vipengele hivyo kama maelewano, tenazaidi
ya maelewano, kuhalalisha kinachoitwa ‘idara maalum’katika Katiba ya
Zanzibar ilioko (Sura ya Kumi). Idara maalumya Zanzibar inajumuisha
Jeshi La Kujenga Uchumi (JKU), KikosiMaalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na
Chuo cha Mafunzo (cha
26
wahalifu)
(ib. 121(2). Rais wa Zanzibar ana mamlaka kamili juu yaidara maalum na
tena kikatiba anaitwa ‘Kamanda Mkuu wa IdaraMaalum’.Rasimu hii ikipita
kuwa sheria kama ilivyo, mimi sitashangaaikiwa Zanzibar itarekebisha
Katiba yao katika ibara ya 26(1)ambayo ilivyo inasomeka: ‘Kutakuwa na
Rais wa Zanzibar ambayeatakuwa Mkuu wa Nchi ya Zanzibar, Kiongozi Mkuu
wa Serikaliya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.’ Baada
yamarekebisho, ibara inaweza ikasomeka: ‘Kutakuwa na Rais waZanzibar
ambaye atakuwa Mkuu wa nchi ya Zanzibar, KiongoziMkuu wa Serikali ya
Mapinduzi, Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi na Kamanda Mkuu wa Vikosi
vya Ulinzi na Usalama.’Na hii haitakuwa kinyume cha Katiba ya Shirikisho
kwa sababu,moja, polisi sio jambo la muungano na, pili, Katiba ya
Shirikishoyenyewe inaruhusu.Vilevile Tanzania Bara wanaweza likaufuata
nyanyo na kuwa navikosi vyao vya usalama na ulinzi. Hali halisi ilivyo,
vikosi hivyovya Bara au Tanganyika vitakuwa na uongozi wa kitaalam,
silahaza kisasa na nguvu zaidi kuliko Jeshi la Polisi la Jamhuri
ambalolitajikuta halina fedha za kujiendesha.Nitatoa mfano mmoja wa
kuonyesha migongano hatarishiinayoweza kutokea katika hali halisi.
Ingawa mfano huu ni wakudhania, sio kama hauwezekani kutokea. Rais wa
Jamhuri kwatathmini yake anaona kuna hali ya hatari katika eneo mojawapo
laBara ambao inahitaji kudhibitiwa mara moja. Kwa mujibu wa ib.81,
baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa,kikao
ambacho hakikuhudhuriwa na Rais wa Bara, anatangazahali ya hatari na
kupeleka kikosi cha FFU kuidhibiti. Utangazwajiwa hali ya hatari sio
jambo la muungano (kinyume na Katibailioko ambayo inasema mamlaka juu ya
hali ya hatari ni jambola Muungano, Nyongeza ya Kwanza). Rais wa Bara
pia anapeleka
27
kikosi chake
cha usalama kudhibiti hali hii na kumtaka Rais waJamhuri aondoe mara
moja kikosi cha FFU. Rais wa Jamhurianakaidi ushauri huu. Kwa vyovyote
vile, kutatokea mgongano kwasababu katika hali halisi vikosi vyote
viwili vina hadhi sawa, kikosicha Bara kwa mujibu wa Katiba ya Bara na
kikosi cha Jamhuri kwamujibu wa katiba ya muungano. Lolote linaweza
kutokea katikahali kama hii ambalo haliwezi kutabirika.
D. Mahakama ya Rufani na Mahakama ya Juu
Mahakama
katika ngazi ya Jamhuri ni mbili, Mahakama ya Juuna Mahakama ya Rufani.
Mahakama ya Rufani ni mahakamainayosikiliza rufani kutoka mahakama kuu
za Washirika kamatulivyozoea isipokuwa sio ngazi ya mwisho. Uamuzi wa
Mahakamaya Rufani unaweza kupingwa katika Mahakama ya Juu na uamuziwa
Mahakama ya Juu ni wa mwisho.Mahakama ya Juu ndio mahakama mpya. Pamoja
na kusikilizarufani zote kutoka Mahakama ya Rufani, ina majukumu
mahsusiya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua mambo matatu ––
kusikiliza na kuamua mara ya kwanza na mwisho mashauriyanayohusu
uchaguzi wa Rais wa Jamhuri;– kusikiliza na kuamua mashauri kuhusu
tafsiri ya Katibaya Shirikisho yanayoletwa na serikali yoyote kati ya
tatuzilizopo;– kusikiliza na kuamua migogoro baina ya serikali
hizoinayoletwa na mmoja wao.Pia ina mamlaka ya kutoa maoni ya kishauri
kwa Serikali yaMuungano au Serikali za Washirika. Rasimu haiko wazi
kwambainatoa maoni pale tu inapoombwa au inaweza kufanya hivyo kwautashi
wake yenyewe.Mahakama ya Juu ina Jaji Mkuu na Naibu wake na majaji saba
28
wengine,
jumla ya majaji wakiwa tisa. Mahakama ya Rufani inaMwenyekiti na majaji
wengine 17. Kwa jumla kuna majaji 27 katikaMahakama za Jamhuri (Sio
mzigo mdogo huu!) Kuna vipengelevinavyosisitiza uwiano wa uwakilishi
kutoka pande mbili zamuungano.Jambo la kutatanisha katika muundo huu ni
hili. Mahakamaya Juu na Mahakama ya Rufani sio miongoni mwa mambo
yaMuungano. Pamoja na ukweli huu, ib.158(3) inaweka mamlaka yakutunga
utaratibu na sababu za rufani mikononi mwa Washirikakwa mujibu wa katiba
na sheria zao. Matokeo yake ni kwambaWashirika wanaweza, wakitaka,
kuamua mashauri yapi yaendekatika Mahakama ya Rufani ya Jamhuri na yapi
yazuiliwe.Kwa mfano, Katiba ya Zanzibar ya 1984 iliopo inazuia kesi
zozotezinazohusika na tafsiri ya Katiba ya Zanzibar, na kesi za
Kiislamuzilizoanzia katika Mahakama za Kadhi kusikilizwa na Mahakamaya
Rufani, hii pamoja na kwamba Mahakama ya Rufani ni jambo laMuungano
(nyongeza ya pili). Inawezekena kabisa kwamba baadaya Rasimu kuwa
sheria, katiba za Washirika zikasema kwamba –– kesi zote za tafsiri za
katiba zao;– kesi zote za uchaguzi pamoja na uchaguzi wa marais wao;–
kesi zote za uhaini dhidi ya serikali zao;– kesi zote sinazohusu
ukiukwaji wa haki za binadamu aumaadili na miko ya viongozi;
n.k.hazitapelekwa katika Mahakama ya Rufani ya Jamhuri na badalayake
zitasikilizwa na kuamuliwa mara ya mwisho na mahakama zaoza rufani au na
jopo la majaji (ya idadi iliyotajwa) wa MahakamaKuu yao. Isitoshe,
wanaweza kwenda mbali zaidi kwa kusemakwamba matokeo ya uchaguzi wa
marais wao hayatapingwa katikamahakama yoyote ile. Wakifanya hivyo, na
hakuna sababu yakisheria kwanini wasiweze, hadhi ya Mahakama za Jamhuri,
pamojana kazi yao, itapungua.
29
Sasa niangaze taasisi nyeti ya Muungano, na hii sio nyingine,isipokuwa Benki Kuu.
E. Benki Kuu
Uchumi
unaotegemea uuzaji na ununuaji wa bidhaa, fedha namzunguko wa sarafu na
uhamishaji wa fedha unakuwa na nafasiya kipekee. Akiba inawekwa kupitia
fedha; uwekezaji unahesabiwakwa fedha; rasilimali zinathaminiwa kwa
fedha. Benki Kuu, angalaukinadharia, ni taasisi nyeti inayosimamia fedha
katika sura zakembalimbali. Majukumu muhimu ya Benki Kuu ni kutoa na
kusimamiasarafu na fedha na mzunguko na uhamishaji wake; kusimamiaujazi
wa fedha (money supply) na amana (bank deposits) katikabenki zote pamoja
na za kibiashara; kutunga na kusimamia sera yakifedha (monetary
policy); kuratibu, kudhibiti na kuhakiki mabenkiya biashara na uwekezaji
katika nchi; kudhibiti mfumuko wa bei,ikiwemo bei ya fedha za kigeni
(foreign exchange rate); na hatimayeni benki ya serikali. Kwa muhtasari
basi Benki Kuu ni mtunzaji,mlinzi, mwangalizi na msimamizi wa fedha za
taifa pamoja na akibaya nchi, ikiwa akiba ya dhahabu au fedha za
kigeni.Kwa maoni yangu, katika nchi na uchumi kama wetu, na ili
kuepukamisukosuko ya fedha, hakuna budi Benki Kuu idhibiti na
kuongozasoko, badala ya kufuata soko. Benki Kuu ikifuata soko bila kuwa
namsimamo kwa mujibu wa sera ya fedha, na mtazamo wa maendeleowa nchi,
basi litakuwa kama bendera inayopepea kwa kuelekezwana upepo badala ya
kudhibiti mwelekeo wa upepo. Benki Kuuinatakiwa kuwa kinu kinachonasa
upepo ili kujijengea nguvu, siobendera inayoyumbishwa na upepo.Kwa
vyovyote vile, huwezi kuwa na Benki Kuu zaidi ya moja katikanchi moja
hata kama ni nchi ya shirikisho. Je, Rasimu inasema ninikuhusu Benki
Kuu?Kwanza, ‘Sarafu na Benki Kuu’ ni jambo la Muungano. Hii ni tofauti
30
na Katiba
ilioko inayosema kwamba, ‘Mambo yote yanayohusikana sarafu na fedha kwa
ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti);mabenki (pamoja na mabenki
ya kuweka akiba) na shughuli zote zamabenki; fedha za kigeni na
usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za kigeni’ ni jambo la
Muungano (nyongeza ya kwanza,jambo la 12). Hii ni pana zaidi, inataja
sio sarafu tu lakini mamboyote yanayohusika na fedha, ikiwemo, bila
shaka, sera za kifedha.Pamoja na hayo inataja usimamizi wa fedha za
kigeni.Pili, Rasimu katika ib. 218 inasema Washirika wanaweza wakawana
benki zao zitakazokuwa na jukumu la ‘kutunza akaunti ya fedhaza serikali
husika, kusimamia Sera za Kifedha na benki za biasharakatika mamlaka
zao.’ Nitarejea kwenye hii hivi punde.Tatu, majukumu ya Benki Kuu
yaliyotajwa katika Rasimu nimanne –‘(a) kutoa sarafu, kudhibiti na
kusimamia mzunguko wa sarafu;(b) kuandaa na kusimamia Sera na Mipango
inayohusiana nasarafu;(c) kudhibiti na kusimamia masuala ya fedha za
kigeni; na(d) kusimamia Benki za Washirika wa Muungano.’Aya (a) na (b)
haina shida kwa sababu zinahusika na sarafuambayo ni jambo la Muungano.
Lakini aya (c) na (d) sio mambo yaMuungano. Kwa kuwa masharti ya Katiba
ya Shirikisho, ambayohayahusiki na mambo ya Muungano, hayawabani
Washirika,inawezekana kabisa Washirika wasitilie maanani aya hizi
nawakafanya shughuli zao kupitia benki zao kama kwamba mashartihaya ya
kusimamiwa na Benki Kuu, na fedha zao za kigenikudhibitiwa na Benki Kuu,
yasingekuwepo.Nitahitimisha na kujumuisha hoja yangu juu ya Benki Kuu
kamaifuatavyo:
31
Moja, Benki
Kuu iliyotajwa katika Rasimu inakosa majukumumuhimu ya Benki Kuu za
kawaida.Pili, benki za Washirika zina uhuru wa kutekeleza mamlaka yoteya
benki kuu isipokuwa kutoa na kudhibiti mzunguko wa sarafu.Kwa hivyo,
Benki Kuu ya Shirikisho ni Benki Kuu kwa jina tu.Ukweli ni kwamba
inafanana zaidi na baraza la sarafu, yaani‘currency board’, kuliko Benki
Kuu.
F. Mapato na Gharama za Muungano
Rasimu
inataja vyanzo vinne vya mapato ya Muuungano (ib. 215).Vyanzo hivyo ni
–‘(a) ushuru wa bidhaa;(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za
Muungano;(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na(d) mikopo
kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.’Aya (a) na (b) zimetajwa
katika mambo ya Muungano. Ushuru
wa bidhaa una utata kidogo. Ninafikiri hii haimaanishi ushuru
wa bidhaa unaosimamiwa na idara ya forodha kwa maana ya
excise duty
. Kwa hivyo labda inamaanisha ushuru au kodi kama
value added tax
(VAT), sales tax, produce cess n.k.
Kama hii ndioiliyokusudiwa inahitaji ufafanuzi zaidi. Kwa vyovyote
vile, ushuruwa bidhaa unakusanywa mahali pa uzalishaji, uuzaji na ulaji.
Kunamasuala mawili hapa. Moja, Serikali ya Muungano itahitaji vyombo
na maofisi katika sehemu mbalimbali za maeneo yote mawili ya
Muungano
kuweza kukusanya ushuru. Hii yenyewe inaweza ikawana gharama kubwa.
Pili, ili kuziba nakisi katika bajeti yake, Serikaliya Muungano
itajikuta kila mara inaongeza ushuru huu, jamboambalo litawaongezea
wananchi mzigo. Pamoja na kulipa ushuruhuu wananchi watakuwa wanalipa
kodi na malipo mengine kwaserikali zao.
32
Inaelekea
ushuru wa bidhaa ndio utakuwa chanzo kikuu chamapato ya Serikali ya
Muungano. Maduhuli inamaanisha karona malipo yanayolipwa serikalini kwa
huduma mbalimbali (k.m.pasipoti, hati ya uraia, visa, n.k.). Kuna idara
moja tu katika mamboya Muungano ambayo inaweza kutoa mapato haya, nayo
ni ‘uraiana uhamiaji’. Kuna usajili wa vyama vya siasa pia lakini hii
inawalakin nitaozungumzia baadae.Ninahisi kwamba mapato makubwa ya
Muungano yatatokana namchango wa Washirika. Ni wazi kwamba Bara ndio
itachangiaasilimia kubwa sana. Inanishangaza kwamba Rasimu haitajikabisa
uwiano wa mchango kutoka kwa Washirika. Jambo hili ni laawali kabisa
kuandikwa katika rasimu yoyote ya Shirikisho.Hili la mkopo kutoka nje na
ndani sina hakika nalo. Serikali ambayohaina chanzo chake huru cha
mapato au sekta ya uzalishaji auwalipa kodi wakubwa, hususan mashirika,
chini yake, itakuwa nahali ngumu ya kupata mikopo.Kwa jumla, kuna
utatanishi na wasiwasi kwa upande wa mapatoya Muungano. Kwa upande wa
gharama, ni wazi kwambakuendesha serikali ya muungano kutakuwa na
gharama kubwa.Kazi inayofanywa na taasisi moja au idara moja katika
muundouliopo sasa itahitaji taasisi mbili. Kwa mfano, badala ya kuwa
naTume moja ya uchaguzi, sasa kutakuwa na tume mbili, moja yaMuungano na
nyingine ya Bara. (Ukiongeza ya Zanzibar kutakuwana Tume tatu za
uchaguzi.) Na hivyo hivyo kuhusu tume nyingine.Ukiangalia juujuu tu,
licha ya taasisi na idara za kawaida katikaserikali, kuna tume karibu
nane na mabaraza mawili yenyewajumbe wazito ambao bila shaka watakuwa na
mishaharaminono na marupurupu poa. Wananchi wamekwishaanzakuonyesha
wasiwasi wao kwa kuwaongezea mzigo wa kubebaserikali kamili nyingine,
zaidi ya hizi mbili tulizonazo.
33
G. Mambo ya Muungano
Kama
tulivyoona, kuna mambo saba katika mambo ya Muungano.Sina mengi ya
kusema zaidi ya yale niliyoyasema kwamba polisi,Mahakama ya Juu,
Mahakama ya Rufani na mambo yote yahusuyofedha na fedha za kigeni
yangefaa kuwa mambo ya Muungano.Kuna jambo moja la Muungano ambalo mimi
binafsi sioni mantikiya kuwa kwenye orodha hii - ‘Usajili wa Vyama vya
Siasa’. Ukiwaumeshaweka muundo wa serikali tatu, jambo linalofuata ni
juuya chama cha siasa chenyewe kama kinataka kugombea uchaguzikatika
eneo moja tu na sio lingine. Kwa hivyo, unaweza ukawa nachama cha siasa
ambacho kinagombea uchaguzi katika Zanzibartu, au Bara tu, au katika
ngazi ya Muungano tu.
H. Michakato ya Katiba na Mengineyo
Kabla
sijaenda kwenye sehemu yangu ya mwisho na kuhitimishaningependa
kutahadharisha kuhusu michakato ya katiba zawashirika. Siku moja baada
ya kuzinduliwa kwa Rasimu tulianzakuwasikia viongozi wachache, na hata
wahariri wa magazeti,wakitoa maoni yao juu ya katiba ya Tanganyika.
Wengine walidirikikusema wala hakuna haja ya kusuburi kupitishwa kwa
Rasimu,maandalizi yaanze mara moja. Wachache, wakiwemo
viongoziwaandamizi, walinukuliwa wakisema wala hakuna haja ya
kupatamaoni ya Watanganyika kwa sababu maoni yamekwishatolewakwa Tume ya
Mzee Warioba. Na wakaongeza kwamba wajumbe waTume ya Warioba kutoka
Tanganyika wanaweza kugeuzwa kuwaTume ya Katiba ya Tanganyika.
(Nisingeshangaa kama mwingineangesema wala hakuna haja ya kuwa na Bunge
la Katiba, Wabungekutoka Bara katika Bunge lililopo wanaweza wakajigeuza
kuwaBunge la Katiba.) Kiongozi mmoja wa serikali, kutokana nabusara na
uzoefu wake, amekaririwa akasema kwamba mchakatowenyewe hautachukua
muda. Kwamba ukianza mara baadaya uzinduzi wa Katiba ya Muungano mwezi
wa Aprili unaweza
34
ukamalizika
Desemba 2014 na 2015 tukawa na uchaguzi waBunge na Rais wa Tanganyika
pamoja na uchaguzi wa Bunge laMuungano na Rais wa Muungano. Mimi binafsi
nilibaki kuduwaakuona jinsi tulivyomeza mwendo wa
fastafasta!Kwanza,
sio sahihi hata kidogo kuzumguzia jambo ambalo hatunauhakika nalo hata
kidogo. Kwa nini tuwachukulie wananchi wetu nikama mbumbumbu ambao
watakubali chochote wanachoambiwapamoja na rasimu hii? Mabaraza
hayajaijadili; wananchi wenyewehawajaijadili ingawa wameanza kutoa maoni
yao, pamoja nahisia zao za hofu na wasiwasi. Rasimu ya pili haijatoka;
hatujuimarekebisho yatakayofanyika. Bunge la Katiba halijaketi.
Hatujuikwamba litapitisha rasimu hii bila mabadiliko, tena makubwa.Kura
za maoni bado.Pili, nani ameamua kwamba mchakato wa kupata katiba
yaTanganyika, ikiwa muundo wa serikali tatu utapita, utafananana ule wa
katiba ya Muungano? Mchakato wa kupata katiba yaTanganyika unaweza ukawa
tofauti kabisa; unaweza ukawa borazaidi na wa demokrasia pana zaidi.
Inawezakana kabisa kwambamchakato wa katiba mpya ya Tanganyika usianze
na tume bali namkutano wa kitaifa wa kujenga mwafaka.Tatu, sio sahihi
kisiasa au kimantiki, kusema kwamba wananchiwamekwishatoa maoni yao, kwa
hivyo hakuna haja ya kurudi kwao.Walipotembelewa na Tume ya Warioba
maoni waliyokuwa wakitoani juu ya katiba ya Muungano, sio ya Tanganyika
wala Zanzibar.Mfano uliokuwa mbele yao ulikuwa wa katiba ya Muungano,
siowa Tanganyika. Labda zaidi ya asilimia 95 wala hawajui kwambatuliwahi
kuwa na Katiba ya Tanganyika. Ni kweli kabisa, maoniyaliyotolewa mbele
ya Jaji Warioba yalikuwa ni manunguniko namatakwa yao. Sasa Tume inasema
haiwezi kushughulikia mambomengi ya msingi, kama vile rasilimali na
madaraka ya umma, kwahoja kwamba katika muundo waliopendekeza mambo haya
ni ya
35
Washirika na
sio ya Jamhuri ya Muungano. Je, nani anajua kwambawananchi wameridhika
na hoja hiyo? Je wananchi wakisemakwamba Rasimu irejeshwe kwenye Tume
ili Tume ifanye kazi yaziada kuutafuta muundo ambao utashughulikia
kikatiba mamboyao ya msingi?Ukweli ni kwamba, kuna mengi hatujui wala
hatuwezi kutabiri,kiasi kwamba kuanza mjadala wa mchakato mwingine
wakati huo
uliopo wenyewe haujafikia tamati, ni sawa na kupiga ramli. Na, nne,
kuna hatari
katika kufanya hivyo. Ni sawa na kuwapotoshea lengowananchi kwa kuanza
mjadala mwingine kabisa na kuwafanyawaache kujadili hili ambalo liko
mbele yao. Sina haja ya kuongezazaidi juu ya suala ambalo ni wazi.Kabla
sijahitimisha nigusie, angalau kwa muhtasari, matumaini yawananchi ya
Tanzania Mpya.
IV.
MATUMAINI YA TANZANIA MPYA
Tulipoanza
mchakato wa katiba mpya, wengi wetu, pamoja nawananchi wa hali ya chini,
tulikuwa na matumaini kwambatutajadili na kujiwekea hatma mpya ya nchi
yetu yenye matumainina mwelekeo unaojali walio wengi, hususan
wavujajasho. Maonimengi yametolewa na wananchi, mengi yakiwa
manunguniko,matatizo na hali ngumu ya maisha kwa jumla. Ilikuwa ni juu
yawajumbe wa Tume, kwa busara zao, na utaalam wao, kufanyauchambuzi,
kuyaainisha maoni na kutafsiri matakwa ya wananchikatika lugha na dhana
ya katiba.Haraka haraka tunaweza kusema kwamba maoni mengi yawananchi
yalijikita kwenye maeneo matatu ya msingi yanayogusamaisha yao kwa
karibu. Moja, ni demokrasia kwa maana yamadaraka ya umma - demokrasia
itakayowawezesha wananchi
36
vijijini na
mitaani kuweza kujiamulia mambo yao wenyewe. Pili, niudhibiti, usimamizi
na uangalizi wa rasilimali na maliasili za taifaili utajiri huo uweze
kuwanufaisha wananchi na vizazi vijavyo.Tatu, ni mpango, mazingira na
taratibu zitakazotoa kipaumbelekwa huduma za lazima na bora kwa wananchi
waliowengi,
kama elimu, afya, maji safi, makazi bora, hifadhi ya uzeeni, na
ajira
stahiki kwa vijana. Kwa jumla, ilitegemewa kwamba Tumeingependekeza
mfumo na muundo wa siasa, utawala, uchumi, namazingira utakaokidhi
matakwa haya.Kwa mfano, madaraka ya umma, kwa maana ya mfumo wa
serikaliza mitaa kuanzia ngazi za chini kabisa kama kijiji, shehia,
mtaana kuendelea, hayajawekewa masharti ya kikatiba.
Rasimuhaikuzungumzia kabisa serikali za mitaa, isipokuwa ibarandogo moja
ambayo inasisitiza kwamba serikali za Washirika‘zitawajibika kustawisha
mamlaka ya wananchi kwa kugatuamadaraka kwa serikali za mitaa
zitakazoanzishwa’ kwa mujibuwa Katiba za Washirika. Hili halina uzito wa
maana kwa sababuinawaachia Washirika mambo muhimu ya kuainisha mfumowa
demokrasia. Hoja ya Tume ni kwamba jambo hilo, pamojana lile la
rasilimali na huduma za elimu, afya n.k. sio mambo yaMuungano na ni juu
ya Washirika kuyashughulikia katika katibazao jinsi wanavyoona inafaa.
Ni vigumu kuikubali hoja hii kwasababu Katiba ya Shirikisho, inatakiwa,
kama katiba mama,kuweka misingi ya mfumo na miundo ya mambo haya ya
msingi.Kitakachofanyika na katiba za Washirika ni kufafanua, kwa
mujibuwa hali yao halisi, bila kuivunja misingi iliyowekwa na katiba
yaShirikisho. Haieleweki kwa nini, kwa mfano, haki za binadamuzimewekwa
kwa ufasaha mkubwa katika Rasimu wakati haki zabinadamu sio jambo la
Muungano. Kwa nini, kwa mfano, tunu,malengo n.k. yame rudiwarudiwa
katika rasimu wakati hizizinaweza zisitiliwe mkazo katika Katiba za
Washirika? Na papohapo hoja inatolewa kwamba madaraka ya umma na
usimamizi
37
wa
rasilimali sio jambo la Muungano na kwa hivyo hayakuguswana rasimu. Hoja
hii, kwa heshima, haina mshiko.Inaelekea tulitarajia mlima, tukapewa
kichuguu. Hata hivyo, labdahatujapoteza yote. Hii ni rasimu ya kwanza,
bado kuna nafasiilimradi tuhakikishe kwamba mijadala juu ya rasimu
haiharakishwina inakuwa huru bila kuingiliwa, na wananchi
kutishwatishwa.Wananchi waielewe vizuri rasimu na maana yake halisi kwa
undaniili waweze kuijadili na kuitafakari kikamilifu na kwa kina.
HITIMISHO
Katika
kuhitimisha mhadhara wangu nitarejea kwenye udhaniau hypothesis yangu.
Nilisema kwamba ninavyodhani mimi,masharti mengi ya Rasimu yalikuwa
maamuzi ya maelewano kwamaana ya compromise na sio mwafaka kwa maana ya
consensus.Baada ya uchambuzi wangu, ninadiriki kusema kwamba
muundowenyewe wa serikali tatu uliopendekezwa ni compromise kati yawale
waliosimamia serikali mbili na wale waliopigania muunganowa mkataba, kwa
maneno sahihi, kuuvunja muungano. Wanaserikalimbili waliona afadhali
kuwa na Muungano, hata kama niwa serikali tatu, badala ya kuuachia
uvunjike; wakajifariji kwamatumaini ya dhamira ya wananchi na nia ya
viongozi.Wana-mkataba wakaona kuwa kwa wakati huu wakubali serikali
tatu wakijua fika kwamba muundo wa serikali tatu hautadumu na
vyovyote
vile utavunjika.Nilisema pia kwamba compromise inazaa uamuzi
legelege.Compromise juu ya muundo, kwa maoni yangu, imezaa muundowa
muungano legelege. Kuna maeneo mengi nimechambuana kudhihirisha kwamba
yatazaa migogoro ambayo hatimayeinaweza kuuvunja Muungano. Kero za
Muungano zitaendelea,safari hii kutoka pande zote mbili.
38
Muungano
ukivunjika hakuna mwananchi atakayenusurika,awe wa Tanganyika au wa
Zanzibar. Tuna mifano mingi ya hivikaribuni. Shirikisho la Sovieti
liliposambaratika, likazaa migogorona vita vya wenyewe kwa wenyewe –
mgogoro wa mpaka kati yaUzbekistan na Krygistan; mgogoro kuhusu maji
kati ya Uzbekistanna Tajikistan; vita vya Chechnya visivyoisha; vita
kati ya Azerbaijanna Armenia, n.k. Waliofaidika ni mashirika ya kibeberu
ambayowalitua kama tai kupora rasilimali za Urusi.Shirikisho la
Yugoslavia lilipogawanyika likazaa vita katika eneolile kiasi kwamba
mpaka leo halijatulia. Wanasiasa wenye uchuwa madaraka wakisukumwa na
nchi za Magharibi, wakatumiauhasama wa jadi kati ya makabila na dini
kushawishi mgawanyiko.Makabila na dini zilizofanya kazi kwa pamoja, kwa
kiasi fulani, chiniya uongozi wa Rais Tito, na mfumo wa Shirikisho,
yakagawanyika.Leo hii nchi ambayo ilikuwa na amani kwa zaidi ya miongo
mitatuimegawanyika katika nchi kama saba (Croatia, Serbia,
Bosnia,Macedonia, Montenigro, Kosovo na Slovenia). Na vita
badovinaendelea. Waliofaidika ni nchi za Magharibi kupitia NATO
yao.Mwandishi mmoja anaweka wazi maslahi ya nchi za Magharibikatika
kusambaratisha Yugoslavia. Nimnukuu kwa sababu mfanohuu una mengi ya
kutufundisha:Beginning in 1990 Germany and the United Statessought and
achieved the breakup of Yugoslaviain two stages—1992-1995 and 1998-1999.
TheGerman government aimed at this division becauseit wanted to include
as territory of its “vital interest”Slovenia and Croatia, the most
economicallydeveloped states of the Yugoslavian confederation. …Through
them Germany would achieve access to theAdriatic Sea.
39
The United
States was interested in the more recentlyestablished states (Bosnia,
Serbia, the former SocialistRepublic of Macedonia), which controlled the
onlyroute from east to west and from north to south throughthe Balkan
mountains. The Balkan area, along withRomania, Bulgaria, Turkey and the
Arab nations, formsa European-Middle East bloc, which the United
Stateswants to control (including the former states of theSoviet
Union—Kazakhstan, Azerbaijan, Turkmenistan,Tajikistan) for the complete
exploitation of the great oilresources of the Caspian Sea.
10
Na hapa,
karibu na nyumbani, Sudan ya Kusini ilipojitengakumekuwa na migogoro juu
ya mafuta, ambayo bado inaendelea.Nimewahi kusema na ninarudia. Suala
la Muungano sio letu tu.Kuna nchi za kibeberu zina maslahi makubwa ya
rasilimali pamojana ya kijeshi katika eneo letu, hasa Bahari ya Hindi.
Tukibezamambo haya nyeti kwa sababu tu ya uchu wa madaraka ya
viongoziwachache, tutawapeleka watu wetu kwenye hali mbaya.
***
Tume
imesema, ingawa hatujaiona taarifa yao rasmi bado, kwambawananchi wengi
walitaka serikali tatu. Lakini, kwa heshima,ningependa kuhoji msimamo
huu. Jukumu la Tume halikuwa tukukusanya maoni na kuhesabu nani amesema
nini. Jukumu laTume lilikuwa ni kupokea maoni, kuyaainisha na
kuyachambuaili kupata kiini chake na sababu zake. Wajumbe walipoambiwa
nawananchi wa eneo moja kwamba wajengewe india ndogondogo,haikumaanishwa
hivyo, bali wananchi walikuwa wanadai hospitali;kwa kuwa viongozi
wanapelekwa India kupata huduma za kiafya,basi wao pia wakataka
wajengewe hospitali bora katika maneneoyao na wote, viongozi na
wananchi, watibiwe humohumo nchini.
40
Hatimaye,
ukiangalia kwa undani kero za Muungano, kwamfano, suala lenyewe sio
idadi ya serikali bali ni la demokrasia.Wazanzibari kwa muda mrefu tu
wamedai haki yao ya kujiamuliamambo yao wenyewe; kushirikishwa katika
maamuzi muhimu;kutokudhalilishwa, na kupewa heshima ya mshirika huru.
Madaihaya ni halali. Hoja yangu kwa muda mrefu ni kwamba
tusiangaliesuala la Muungano kwa jicho la idadi ya serikali bali kwa
mtazamowa demokrasia. Na tukifanya hivyo tunaweza kubuni muundowa
kipekee kutokana na historia yetu na hali halisi ya Washirikakutokuwa na
uwiano wa uchumi, eneo au idadi ya watu.Muundo wa serikali tatu, au
shirikisho kama unaoainishwa,unajikita kwenye usawa wa kisiasa
(political equality). Kwa msingihuu, uwakilishi, hususan katika vyombo
vya kuchaguliwa, haunabudi uwe sawa bila kujali idadi ya watu. Lakini
katika hali yetuya uchumi, mchango wa Washirika katika gharama za
shirikishohauwezi ukawa sawa, wala sio haki, kwa sababu hatuna usawa
wakiuchumi. Kwa vyovyote vile, Tanzania Bara itachangia asilimiakubwa ya
gharama za Shirikisho. Hatimaye, anayelipa mpigazumari ndiye
anayechagua wimbo.Kwa maoni yangu, kama tungekuwa na mtazamo wa
kidemokrasiatungeweza kubuni muundo ambao unakidhi matakwa ya pandezote
mbili bila hatari ya kuuvunja Muungano. Mimi binafsinimewahi kutoa
pendekezo la muundo mbadala. Mara ya kwanzaniliwasilisha pendekezo langu
kwa Baraza la Wawakilishi kamamiezi michache iliyopita. Kwa muhtasari,
nilipendekeza dolakamili mbili, la Zanzibar na la Muungano. Bunge la
Muunganolitakuwa na mabaraza mawili, Baraza la Wananchi na Baraza
laNchi. Wajumbe wa Baraza la Wananchi watachaguliwa mojakwa moja na
wananchi wa pande zote mbili kutoka majimboni.Baraza la Nchi litakuwa
dogo lenye, tuseme kama wajumbe 30,15 kutoka Bara na 15 kutoka Zanzibar
wakichaguliwa na Bunge
41
la Zanzibar
na wabunge kutoka Bara katika Baraza la Wananchiilimradi wasiwe wajumbe
wa bunge lolote lile. Na nilipendekezaorodha tatu – moja ya mambo ya
muungano, nyingine ya mamboya kushirikiana (concurrent matters) na
orodha ya tatu ni juuya mambo ya pamoja (joint interest). Kutokana na
muda siwezikufafanua; nia yangu ni kudhihirisha kwamba muundo
mbadalaunawezekana.Rasimu imezinduliwa. Imeanza kujadiliwa. Tuchukue
nafasi hiikuijadili kwa makini ili hatimaye malengo na matumaini ya
waliowengi yatimizike.
Makamu Mkuu wa Chuo, wanakigoda wenzangu, rafiki zangu na
wageni
waalikwa. Mhadhara huu ulikuwa ni mchango wangu wamwisho katika wadhifa
wangu wa Nyagoda wa Mwalimu Nyererelakini, nikiwa na uzima wa afya,
hautakuwa mchango wangu wamwisho katika mijadala ya kitaifa.Nawashukuru
sana kwa kunisikiliza. Ahsanteni na kila la heri.
Post a Comment