Ratiba ya Ligi Kuu soka nchini Uingereza imetoka leo(Juni 19,2013) Huku Mabingwa Manchester United na mwanzo mgumu dhidi ya Liverpool na Manchester City ndani ya mechi tano za Mwanzoni.

Mabingwa Manchester United.


Ratiba  ya Ligi Kuu soka nchini Uingereza imetoka leo(Juni 19,2013)  na mechi ya kwanza ya David Moyes nyumbani kama kocha mpya wa Manchester United itakuwa dhidi ya Cheslea yenye kocha mpya pia, Kocha Jose Mourinho.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu, Manchester  United watakuwa na mwanzo mgumu katika ligi hiyo msimu ujao 2013-14 wakisafiri kuwafuata Liverpool na Manchester City ndani ya mechi tano za mwanzoni.


Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa  Manchester City,Kocha Manuel Pellegrini, ni Nyumbani Uwanja wa Etihad kwa kucheza na Newcastle.


Kocha David Moye.
Manchester  United itaanza na mabingwa wa Kombe la Ligi, Swansea Agosti 17, kabla ya kurejea nyumbani kumenyana na Mourinho na Chelsea yake Old Trafford wikiendi inayofuata. 




Mechi na Liverpool itafuatia Agosti 31 kabla  Dabi ya kwanza ya Jiji la Manchester itachezwa hapo Septemba 21 Uwanja wa Etihad kati Manchester  City na Manchester  United na Marudiano ni Old Trafford Machi 1.




Arsenal wataanza Msimu wao wakiwa Nyumbani Emirates kwa kucheza na Aston Villa huku Liverpool pia wakiwa Nyumbani kuivaa Stoke City na Tottenham wataanza Ugenini dhidi ya Timu iliyopanda Daraja Crystal Palace.





Zilizopanda:Hull (Picha Juu ) na Cardiff (picha chini) zote zitacheza nyumbani mechi za kufunga msimu wa Ligi kuu Uingereza 2013/2014.


MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND 2013/2014 ni  (AGOSTI 17,2013).


Arsenal v Aston Villa


Chelsea v Hull City


Crystal Palace v Tottenham Hotspur


Liverpool v Stoke City


Manchester City v Newcastle United


Norwich City v Everton


Sunderland v Fulham
 

Swansea City v Manchester United


West Bromwich Albion v Southampton


West Ham United v Cardiff City

Post a Comment

Previous Post Next Post