Kwa
mujibu wa mwanasaikolojia mashuhuri nchini Ireland, watu wanaoamini
dini kwenye nchi nyingi zilizoendelea watakuwa wachache mno ifikapo
mwaka 2041.
Utafiti kuhusu imani ya watu wanaoishi katika nchini 137 ambao
umetengeneza kitabu chake kipya, umegundua kuwa upagani unazidi
kuongezeka zaidi kwenye nchi zilizoendelea kutokana na utajiri.
Utafiti huo umeelezea pia imani maarufu kuwa watu wenye dini
watawatawala wapagani kwakuwa wao (watu wa dini) huzaa watoto wengi.
Dr Nigel Barber amekiita kitabu chake, ‘Why atheism will replace religion,’ (Kwanini upagani utachukua nafasi ya dini).
Amesema wapagani wengi wapo kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi na
dini itapungua kwa watu kutokana na kuongezeka kwa utajiri wa mtu mmoja
mmoja.
Kitabu hicho kinaandika kuwa watu hawatategemea tena nguvu za miungu
kwakuwa mali walizonazo zinamaliza shida zao zote.Mwandishi huyo anadai
kuwa dini inapungua si tu kwasababu watu wanakuwa matajiri bali pia ni
kutokana na kuongezeka kwa ubora wa maisha, kupungua kwa magonjwa
hatari, elimu nzuri na ustawi mzuri wa maisha.
Anaamini kuwa hakuna haja kubwa ya dini kwenye jamii kama za Japan na
Sweden ambako watu wa kawaida tu wameridhika na watu wengi wana mali.
Dr Barber amesema dini ilizalishwa na mababu zetu ambao walikumbwa na
changamoto nyingi katika maisha yao.
Maelezo kwenye kitabu hicho yanasema:
‘Dini ilizaliwa kuwasaidia mababu zetu kukabiliana na woga na
wasiwasi.Imani kuhusu Mungu inapungua pale ambapo watu wa kawaida
wanafurahia maisha, wana usalama katika afya na mambo yao ya fedha. Hata
Facebook inaiua dini sababu inatoa majibu ya woga wa dunia ambao dini
haina majibu yake.’
Takwimu ya watu wasiomani uwepo wa Mungu duniani kwa mujibu wa Psychology Today
There is almost no Atheism in Sub-Saharan Africa
But there are more atheists in Europe:
64% of people are non-believers in Sweden
48% of individuals are atheist in Denmark
44% of French citizens do not subscribe to a religion
42% of Germans do not believe in a god.
64% of people are non-believers in Sweden
48% of individuals are atheist in Denmark
44% of French citizens do not subscribe to a religion
42% of Germans do not believe in a god.
By Daily Mail
Post a Comment