Majibu kutoka kwa Batuli mwenyewe Baada ya sms kusambaa ikisema muigizaji Batuli anaumwa sana anahitaji msaada, haya hapa

Siku chache zilizopita kulikuwa na ujumbe wa sms ukisambaa kwa njia ya ku-forward ukisema kwamba muigazaji Zaytun Kibwana a.k.a Batuly anaumwa sana anahitaji msaada. Kama ilivyokawaida kwa wasanii wengi kuna utaratibu wa kusaidiana wakati matatizo kama haya. Watu wengi walijua Batuli huyu ndiyo mwenye jina halisi la “Yobnesh Yussuph” ambaye ndiye maarufu sana kwenye bongomovie. Kumbe kuna msanii mwingine anaitwa Zaytun Kibwana na yeye pia anatumia a.k.a Batuly ndiyo alikuwa anaumwa.

Kutoka na sms ile watu wakaanza kupigia simu Batuli lakini majibu waliyokutana nayo ni tofauti walivyotegemea kwasababu Batuli alikuwa haumwi. Hiki ndicho alichosema Batuli kuhusu hii ishu, “Binti unaejiita Zaytun Kibwana a.k.a Batuly yawezekana jina langu umelipenda sana au umeona ndio njia ya kutokea kisanaa maana nitacomplain na kitakachofuata utajulikana, Mimi nadhani hutafanikiwa kwa style hii uitakayo hakuna Shortcut katika maisha. Unapotumia a.k.a yangu halafu unaoomba msaada unategemea kupata kweli? Umetumia jina langu kila anaenitafuta namwambia sio mimi hivyo msaada unakosa na unaonekana tapeli wakati una matatizo unatakiwa usaidiwe, tumia akili ili upate msaada. Kutumia Nick Name yng ni kujipotezea wakati na hutafikia malengo.”

Post a Comment

Previous Post Next Post