MBUNGE KIGOLA AWATAKA WALIMU WAGOME KUFUNDISHA WANAFUNZI WANOKAA CHINI

Mbunge Kigola


 Jesca Msambatavangu mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa( wa  saba kutoka kushoto waliokaa) aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi  wa mpango  wa  kusomesha  sekondari wanafunzi wasio wanaotoka familia zisizo na uwezo  ujulikanao kama Mufindi Scholarship Program (MSP),akiwa na  viongozi mbali mbali wa mradi huo ,wakuu  wa  shule za sekondari na 18 wilaya ya  Mufindi, wanafunzi  waliochaguliwa  kusaidia kusomeshwa na mbunge wa  jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola( wa tatu kulia  waliokaa)
Wakuu  wa shule  za sekondari Mufindi mkoani Iringa  wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mufindi Scholarship Program (MSP),mgeni rasmi  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu wa sita  kulia na mbunge wa  jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola wa nne kulia
 Wanafunzi  wa Mdabulo  sekondari  wakifurahi kwa kucheza muziki

 Mratibu wa Mufindi Scholarship Program (MSP)



 Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu akisalimiana na baba mzazi wa  George Kavenuke  Kulia




Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola amewataka  wakuu  wa  shule na  walimu katika   wilaya ya Mufindi mkoani Iringa  wasikubali kufundisha  wanafunzi wanaosomea chini ya ardhi .

Mbunge  huyo alitoa kauli  hiyo jana katika  ukumbi  wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi wakati wa hafla ya  uzinduzi  wa mpango  huo kuwasomesha  watoto 81 elimu ya  sekondari unaojulikana kana  Mufindi Scholarship Program (MSP)ulioanzishwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya  Muyodeso na Shalom Center .

Pamoja na mbunge  huyo  kupongeza  jitihada za mashirika  hayo kwa  kusaidia  elimu watoto hao  wanaotoka familia masikini ila bado alisema  kuwa  kutokana na wilaya ya Mufindi  kuongoza kwa kilimo  cha miti  na kuwa na msitu  mkubwa wa Taifa  msitu  wa Sao Hill kamwe asingependa  kuona  walimu  wanaendelea  kulia na uhaba wa madawati na  hivyo kuwataka  walimu kususa  kufundisha madarasa ambayo  wanafunzi   hawana madawati ya  kukalia.

" Nawaombeni  walimu  kuanzia sasa msikubali kufundisha wanafunzi  wanaokaa chini ....nawaomba  kila mkuu  wa  shule kutoa ripoti ya hali halisi ya madawati katika shule yake kwa afisa  elimu wa  wilaya  ili kuwezesha kila shule  kuwa na madawati "

Alisema  wilaya ya Mufindi ina utajiri mkubwa wa  miti  hivyo haipendezi  kuona  wanafunzi wanakosa madawati ya  kukalia na  wanasomea ardhini .

Kwani  alisema kwa upande  wake kama mbunge ameanza  kulitafutia ufumbuzi suala  hilo na amepata  kutoa msaada wa madawati katika  shule mbali mbali za   jimbo lake  na  kuwa  jitihada kama  hizo  pia  zimefanywa na mbunge mwenzake wa  jimbo la Mufindi kaskazini .

Akielezea  kuhusu msaada  wa mashirika hayo mawili yasiyo ya  kiserikali ya Shalom Center  na Muyodeso ambayo yamejitolea   kuwasaidia  elimu ya sekondari  watoto 81   katika  wilaya ya  Mufindi  alisema jitihada  hizo  zinapaswa  kuungwa  mkono na serikali kwa  kusaidia fedha  zaidi asasi  hizo ili  kuendelea  kutoa msaada kwa  watoto hao.
mwenyekiti  wa kamati ya maandalizi ya mpango  huo George Kavenuke alisema mpango  huo  umelenga  kuwasaidia  watoto wa  wilaya ya Mufindi ambao  wanauwezo mkubwa darasani ila  wanashindwa  kuendelea na masoni  kutokana na kutoka katika familia masikini .

Kavenuke  alisema  kuwa mradi huu unatekelezwa na Mashirika mawili ambayo ni Muyodeso na Shalom centre for street children ambapo Shalom atakuwa Shirika Kiongozi (lead Organization) na Muyodeso ikiwa ni asasi shiriki katika mpango  huo.

Alisema  kuwa katika  kutekeleza maradi  huo  mashirika hayo yamelenga  kuwasaidia  vijana 420 ambapo  kiasi cha  Tsh milioni 88,200,000 zinahitajika  kwa hadi  mwaka mwaka 2015 kwa  ajili ya kuwalipia ada na michango mbalimbali ya shule kutoka  kidato  cha tatu  hadi cha sita

"Mradi unalenga pia kuwahamasisha wadau wengine kuona umuhimu wa kutoa misaada na huduma kwa vijana watokao katika familia masikini katika shule za Kata na ambao uwezo wao wa kufaulu ni wa kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu..Kwa Mwaka huu 2013, tunatarajia kuwahudumia vijana 81 ambao wamefaulu ambapo jumla ya shilingi 17,010,000 zinahitajika ili kuweza kuweza kugharamia ada, michango, vitabu na sare  za  shule"

Hata  hivyo  alisema  kuwa uwezo wa Mashirika hayo ni kuwalipia ada na michango mbalimbali ya kawaida na mithihani. hivyo bado wanaomba jamii kujitokeza kusaidia  zaidi vijana hao kupitia mpango  huo 

















Akielezea utaratibu  uliotumika  kuwapata  wanafunzi hao watakaoanza kunufaika na mpango  huo  alisema mbali ya  kuwashirikisha  wakuu  wa  shule na  wadau  wa  elimu  ila bado ilitungwa mitihani ya Masomo saba, kufanywa, kusahihisha  ambapo jumla ya  vijana  zaidi ya 100 walioteuliwa  kutoka  shule zaidi ya 17 walifanya mtihani  huo ila vijana  hao 81 ndio  waliopata ufaulu mzuri  zaidi

Post a Comment

Previous Post Next Post