TAARIFA YA SERIKALI
Ndugu Wananchi,
Jana majira ya saa moja usiku, nchi yetu imekutwa na tukio la kusikitisha sana la kushambuliwa kwa kumwagiwa tindi kali watalii vijana wawili raia wa Uingereza Kate Gee na Kirstie Trup wwote wakiwa na umri wa miaka 18. Shambulizi hilo lilifanyika katika eneo la Shangani. Tukio hilo ni kubwa na linashitua sana kwani limeanza kuchukua sura mpya kutokana na tindi kali kuanza kumwagiwa wageni.

Kumwagiwa vijana hao tindikali hakuwezi kuachiwa hata kidogo kwani
kitendo hicho kinajaribu kuiondoshea nchi sifa iliyojijengea ya Zanzibar
kuwa ni eneo la Amani na Utulivu. Mbali hayo, tendo hilo halikubaliki
katika mazingira ya kibinadamu kwani kila binadamu ana uhuru wa kuishi
na kutembea akiwa ana uhakika na usalama wake. – Sisi wenyewe
Wazanzibari, tunatembea na kuishi nchi mbali mbali za kigeni.
Kuachwa kuendelea kwa vitendo vya aina hii kunaweza kuwajengea hofu
wageni na raia wetu. Aidha, kitendo hicho kinaweza kuathiri sana sekta
ya utalii ambayo ni sekta kiongozi katika muhimili wa uchumi wetu.
Katika kuhakikisha jambo hilo halipewi nafasi kuendelea tena,
serikali imekusudia kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kuendesha uchunguzi
mkali wa kuwasaka wahusika ili kuweza kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.Vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikifanya kazi kwa pamoja
kuwatafuta wahal;ifu hao na mara watakapokamatwa watafikishwa kwenye
vyombo vya sheria. Katika kufanya kazi hiyo Serikali inawaomba wananchi
kutoa ushirikiano utakaopelekea kuwakamata na kuwafikisha katika vyumba
vya sheria wote waliohusika na tukio hilo. Serikali ya Zanzibar kwa
upande wake inaahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa yeyote
atakayesaidia kukamatwa kwa watu waliofanya uhalifu huo.
Ndugu Wananchi,
Kwa vile bidhaa ya tindi kali katika siku za hivi klaribuni imeanza kutumika vibaya, Seikali inachukua kila hatua kudhibiti matumizi ya bidhaa hiyo kwa kudhibiti uingizaji, usambazaji, upatikanaji na utumiaji wa tindi kali na inazitaka taasisi zote zinazohusika zitimize wajibu wake kwatika matumizi ya tindikali kwa kutumia sheria iliyopo na kwa haraka kutunga kanuni za kuthibiti uuzaji na matumizi ya tindikali.

Katika kuhakikisha vitendo vya uhalifu haviendelei na hasa katika
maeneo ya utalii yakiwemo maeneo ya Mji Mkongwe na kwenye maeneo ya
fukwe, Serikali inachukua hatua za makusudi za kuweka ulinzi
utakaosaidia wageni wetu kuja nchini na kutembea bila ya bughudha.
Kupitia kauli hii, Serikali inaomba wananchi wote kutoa ushirikiano
mkubwa katika kulinda sekta ya utalii kama ndio chanzo kikubwa cha
uchumi wa nchi yetu.
Hivyo, kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tunatoa pole
kwa waliojeruhiwa na familia zao na tunawaombea waliojeruhiwa wapate
nafuu haraka. Aidha, tunatoa pole kwa ubalozi wa Uingereza nchini
Tanzania na kuuomba watupelekee masikitiko ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa Serikali ya Uingereza kwa tukio hilo na kwamba tutafanya
kila jitihada matukio kama haya yasitokee tena.
Post a Comment