
Mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja Wa
Mataifa inayosimamia Dawa za Kulevya umeanza jana tarehe 13 March, 2014
katika Makao Makuu ya Kamisheni hiyo Vienna International Conference
Center nchini Austria. Mkutano utajadili mikakati ya kupambana na
uzalishaji na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani.
Zanzibar imewakilishwa katika mkutano
huo na Waziri Wa Nchi OMKR Mhe. Fatma A Ferej, Katibu Mkuu OMKR Dr. Omar
Shajak na Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Uratibu na Udhibiti Wa Dawa za
Kulevya Zanzibar ACP Kheriyangu M Khamis
إرسال تعليق