THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar
wamempongeza na kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ufafanuzi na kuunga
mkono hotuba yake kwa Bunge la Katiba aliyoitoa tarehe 21 Machi, Mjini Dodoma.
Wazee hao wamefika Ikulu ya Dar es Salaam leo
jioni , tarehe 9 Aprili,2014 na kuelezea
furaha yao kwa Rais Kikwete.
“Wazee
wote tunakushukuru, tumefurahishwa sana na Hotuba ile kwani umetoa ufafanuzi wa
mambo mengi, kwa hivyo tumefika hapa kukufahamisha kuwa tumefurahishwa sana,
tuko pamoja nawe kwa hali ya aina yeyote “ wamesema
na kumueleza Rais kuwa wanayo mabaraza katika Wilaya, Mikoa, Kata na hata
Mashina.
“Tumefurahi sana , hotuba hii imetufungua na
tumefunguka hivyo tunakuunga mkono na
tuko nawe katika hoja ya Serikali mbili kama ilivyo katika Chama Chetu.” Wazee
hao waliongozwa na Bi. Khadija Jabir Mohammed ambaye ndiye kiongozi wao na Bw.
Waziri Mbwana Ali Katibu wa Wazee. Wazee wengine waliofika Ikulu ni Bw. Juma Ame Juma, Bw. Mohammed Khamis Haji,
Bw. Juma Khamis Khamis na Bw. Tabib Omar Makungu. Wengine ni Alchui Khamis Alchui, Bw. Abdallah
Rashid Abdalla na Bw. Haji Machano Haji.
Rais
amewashukuru Wazee hao kwa kumtia moyo kwa kufika Ikulu kuelezea hisia zao
ambapo Rais amewaeleza Wazee hao kuwa takwimu zote alizotumia katika Hotuba
yake amezitoa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Warioba na kwamba hata maswali
aliyokuwa akiuliza, alikuwa akiyauliza kwa nia ya kuyatafutia majibu na
majawabu ya misingi kama yalivyoandikwa kwenye rasimu ya Tume.
“Takwimu
zote nimetoa kwenye taarifa ya Tume, Maswali niliyouliza nimeyatoa kwenye
taarifa, pia kuna mambo ya uandishi ambayo hayakuwa yameandikwa sawasawa hivyo
nina wajibu wa kutoa tahadhari kwa wajumbe wa tume ili kuwa na uhakika wa dhana
na tafsiri zilizomo kwenye rasimu ya Tume” Rais Kikwete amefafanua
zaidi.
Mwisho!
Imetolewa
na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9
Aprili, 2014
Post a Comment