Mcheza tenisi Elena Baltacha amefariki dunia ikiwa ni miezi
michache tangu alipotangaza kuwa amegundulika na maradhi ya kansa ya
ini.
Mchezaji huyo wa zamani namba moja kwa ubora wa uchezaji mchezo huo
nchini Uingereza inasemakana kuwa amekuwa akipambana na maradhi hayo
muda mfupia tangu habari za kuonekana na ugonjwa huo zilivyo anza
kuzagaa mwezi machi.
Usiku wa jana habari zikatolewa kuwa amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 30 huku mumewe ambaye wametoka kufunga ndoa hivi karibuni
kuonekana kukosa amani baada ya taarifa hizo.
Kipaji: Raia huyo wa Uskochi alikuwa ameshafikia katika kiwango cha nafasi ya 49 ya ubora duniai mwaka 2010
Katika taarifa iliyotplewa kwa niaba ya familia yake wakala wake amesema
'Ni huzini kubwa tunawaletea taarifa hizi Elena Baltacha amefarikia
mapema Jumapili kutokana na maradhi ya kansa ya ini amefarikia akiwa na
umri wa miaka 30.
'Elena, ambaye mara nyingi alikuwa akiitwa kwa jina la utani Bally,
aligundulika na kansa katikati ya January 2014, miezi miwili baada ya
kustaafu kucheza mchezo wa kulipwa na ni siku chache baada ya kuingia
kwenye ndoa na Nino Severino ambaye ni kocha na swahiba wake wa siku
nyingi.
Post a Comment