Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, alisema hayo
jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu upotoshaji
unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari.
Mwambene alisema Serikali haina ugomvi na Jaji Warioba na pia inamheshimu sana.
"Kuna baadhi ya taarifa zina mkanganyiko, zinaonesha kama Serikali
imempa nishani Jaji Warioba kwa kumkejeli, jambo ambalo si kweli,
Serikali inamheshimu," alisema Mwambene.
Alisema nishani aliyopewa Jaji Warioba, haihusu mchakato wa Katiba,
ambao kuna baadhi ya taarifa za mchakato huo, ambazo zimekuwa zikieleza
kuwa baadhi ya wajumbe wanamtukana Jaji Warioba.
"Serikali imempa nishani kwa sababu anastahili, wala haihusu mchakato
huu wa Katiba, hata kama mtu anakinzana na Rasimu ya Jaji Warioba
haimaanishi kamtukana, bali katoa mawazo yake na iliyopo ni rasimu na si
Katiba," alisema.
Mwambene alisema kuwa nishani hiyo, mbali na Jaji Warioba, pia ilitolewa
kwa viongozi wengine akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye
kama heshima ya kuuenzi Muungano.
إرسال تعليق