Yanga watoa masharti mawili kwa Waghana

Hans van Der Pluijm.
 
SIKU chache baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, kurejea nchini akitokea Ghana alikokuwa ameenda kwa ajili ya kutafuta wachezaji, Yanga wametoa masharti magumu.
Kocha huyo ambaye baada ya mkataba wake na Wanajangwani hao kumalizika, aliamua kutimka zake, alisema anakwenda huko kwa ajili ya kuitafutia timu hiyo wachezaji watakaoziba nafasi ya Didier Kavumbagu na Frank Domayo waliotimkia Azam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, amesema kuwa, mara baada ya Pluijm kurejea hapa nchini Jumapili iliyopita akitoka Ghana, wamempatia masharti ambayo anapaswa kuyazingatia kabla ya kuwasajili wachezaji hao ambao kocha huyo alifanya nao mazungumzo.
Alisema Yanga kwa sasa inahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka lakini pia wasiwe na gharama kubwa.
“Kocha amarejea Jumapili alfajiri kutoka Ghana alikokuwa amekwenda kwa ajili ya kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji tunaotaka kuwasajili kwa lengo la kukiimarisha kikosi chetu.
“Hata hivyo, kabla ya kuwasajili kuna mambo mengi ambayo tumeyaangalia na tayari tumeshampatia kocha masharti yetu kabla ya kumalizana na wachezaji hao.
“Tulimwambia tunataka wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini wasiwe na gharama kubwa na waendane na uwezo wetu wa kiuchumi,” alisema Njovu na kongeza kuwa Pluijm amewataka wasiwe na wasiwasi kwa sababu anaijua vizuri Yanga na atafanya usajili huo kwa kuzingatia hayo yote.
- GPL

Post a Comment

أحدث أقدم