Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na
chama hicho, ilieleza kuwa katika siku hizo mbili, pia wajumbe watapokea
na kujadili taarifa ya hali ya siasa nchini; uchaguzi wa ndani ya chama
na taarifa ya fedha, mpangokazi na bajeti.
Kikao
hicho cha kawaida ni cha siku mbili na pamoja na mambo mengine
kitakajadili masuala ya mchakato wa Katiba mpya na rufaa zilizokatwa na
wanachama wake.
Aidha pia, wajumbe
watajadili mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, kanuni na miongozo ya
mabaraza ya chama hicho, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
إرسال تعليق