KUANGUSHWA KWA NDEGE YA MALAYSIA AIRLINE BADO HAIJAJULIKANA NI NANI ANAHUSIKA NA UNYAMA HUU

Hii ndio ndege iliyotunguliwa na kombora ilipokua inavuka mpaka wa Urusi na kuangukia mashariki ya Ukraine na hii picha imepigwa na mmoja wa abiria aliyekuwemo kwenye ndege hiyo wakati wakielekea kuipanda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Asterdam nchini Uholanzi  na kuiweka kwenye ukurasa wake wa facebook na kuandika maneno haya" kama hii ndege itapotea hivi ndivyo inavyoonekana.

Ndege ya shirika la ndege la Malaysia iliyotunguliwa mapema ya alhamisi July 17, 2014 ilipokua ikivuka mpaka wa Urusi kuelekea Ukraine na baadae kuangungia mashariki ya Ukraine na abiria wote wakiwemo wahudumu wa ndege hiyo kupoteza maisha. Ndege hii flight # MH 17 iliyokua akifanya safari zake kutoka Amsterdam, Uholanzi kuelekea Kuala Lumpur, Malaysia ilipigwa na kombora maeneo hayo ya mpaka wa Urusi na Ukraine na baadae kuangukia mashariki ya Ukraine wakati ilipokua atitudi za futi 33,000.
Kipande cha bawa la ndege hiyo

Mpaka sasa hakuna kikundi au nchi yeyote kati ya Urusi au Ukraine iliyokubali kuhusika na  udunguaji wa ndege hiyo ambayo ilikua na jumla ya watu 298. Wataalam wa maswala ya anga wamesema ndege hiyo ilipita nje ya njia yake ya kawaida kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwenye njia yake iliyokua
ianatakiwa kupita,  hiyo ni kawaida kwa ndege nyingi kubadili njia kutokana na hali ya hewa inapobadilika kwa ajili ya usalama wa abiria na ndege hiyo ilipita nje ya njia yake ya kawaida kwa umbali wa maili 200.
Waokoaji wakijaribu kuzima moto.

Wengi wanasema kombora lililotumika kuidungua ndege hiyo ni yale yanayotengenezwa nchini Urusi yenye uwezo wa kusafiri maili 2,684 kwa saa na ndege kama hiyo ya malaysia husafiri kwa maili 560 kwa saa na Wataalam wa maswala hayo ya makombora wameongezea kwamba makombora hayo hayawezi kuendeshwa na mtu mmoja lazima iwe kikundi na yanauwezo wa kusafiri hadi atitudi za futi 72,000 na yenye urefu wa futi 16 na uzito wa paundi 1,500
Kipande kingine cha ndege hiyo kikiwa kimedondoka karibu na magazi ya watu

Abiria kwenye ndege hiyo walikua 283 na 15 walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo ambayo ilianza kumeguka vipande kabla haijafika chini na watu waliofika kwenye tukio wa walikuta abiria wengine wamekufa huku wameshikilia vitambaa vyeupe huku pasi zao za kusafiria zikiwa zimezagaa chini pamoja na mabeki yao.
Kipande kingine cha ndege hiyo kikiwa kimedondoka karibu na ndege hiyo ilipokua umeangukia.

Ndani ya wiki hii zimetunguliwa ndege tatu eneo hilo lakini hazikua ndege za abiria na hii ni kutokana na mapigano ya vikundi yanayoendelea kwenye mpaka huo wa Urusi na Ukraine na lawama nyingi zinaiendea nchi ya Urusi ambapo Rais wa nchi hiyo aliongea mapema leo na kuonekana kuitupia lawama Ukraine lawama ambazo zilipigwa vikali na waziri mkuu wa Ukraine kwa kueleza kwamba ndege hiyo imetunguliwa kwenye mpaka wa Urusi ikielekea kuvuka kuingia Ukraine.


eneo la tukio linavyoonekana.
Wakati ndege hii inatunguliwa kulikuwa na ndege zingine sita za abiria angani eneo hilo. Usafiri wa anga wa Marekani ulishapiga marufuku kwa ndege za nchi hiyo za abiria kupita eneo hilo..

Post a Comment

أحدث أقدم