HAKIKA
maji yanafuata mkondo. Huyu ni Asia Mzinga (pichani juu) binti wa
mwimbaji mkongwe wa taarab Bi Mwanamtama Amir. Hapa ameshuka na bonge la
wimbo.
Baba
mzazi wa Asia Mzinga anayekwenda kwa jina Hamis Mzinga nae pia ni
mwimbaji na mtunzi maarufu wa muziki wa taarab akiwa amepata kutamba na
kundi la Egyptian. Moja ya wimbo uliotamba sana wa Hamis Mzinga ambaye
kwa sasa anaishi Uingereza ni “Mazao Bora shambani”.
Kwa Asia Mzinga hii
inakuwa ni mara yake ya kwanza katika historia yake ya kimuziki
kurekodi wimbo wa taarab. Mwenyewe amesema kuwa shukran za
dhati zimwendee Isha Mashauzi kwa kumfungulia ukurasa mpya kwenye maisha
yake.
Wimbo
huu umepewa jina la “Ubaya Haulipizwi” utunzi wake Isha Mashauzi. Wengi
waliokuwa wakiusikia ukumbini wimbo huu waliuzoea kwa jina la Wema
Hauozi lakini jina halisi la wimbo ni Ubaya Haulipizwi.
Umerekodiwa
katika studio za Soft Records chini ya producer Pitshou Mechat Shemesha
ambaye pia ndiye aliyekung’uta mpini wa solo gitaa.
Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto wakati bass limepigwa na Jumanne Mussa (J Four - Jonh Cena).
Ni
wimbo mtamu wa dakika 8 wenye ujumbe mzuri ndani yake ambao unatosha
kuwa jibu tosha kwa wale wote wanaoipiga madongo Mashauzi Classic. Ni
majibu ya kistaarab yanayoashiria kuwa watu wanataka kufanya kazi na
hawana muda wa malumbano.
إرسال تعليق