MWIMBAJI wa Malaika Band Adaya
Nzinga (wa pili kutoka kulia pichani juu), amefariki dunia Jumapili
jioni katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Adaya Nzinga alilazwa hapo kwa siku kadhaa, tatizo kubwa ikiwa ni malaria kali iliyopanda kichwani.
Bado
haijaelezwa mazishi yatafanyika wapi na lini. Wakati msiba huu
unatokea, bendi yake ya Malaika ilikuwa mjini Morogoro katika onyesho la
Christian Bella “Nani Kama Mama Tour”.
Mashabiki kadhaa wamehoji juu ya bendi hiyo kuendelea na onyesho wakati msanii wao amefariki.
Mdau mmoja anayekwenda kwa jina la Michael Mpiana Safari ameandika kwenye ukurasa wa facebook wa rapa wa Malaika ToToo Ze Bingwa: “Huo
ni msiba mkubwa sana hasa kwenu wanamuziki na washabiki pia… sitaki
kuamini kama viongozi na wamiliki wa band wametoa ‘go ahead’ ya show
kuendelea huku msiba ukitokea kabla ya show kuanza rasmi.
“Najua
wamiliki wa band wao wataangalia hasara watakayopata kama wakikatiza
hii show kufanyika,, lakini kiutu sio ustaharabu na staha nzuri ya
kiafrika kuendelea na burudani huku mwenzenu akiwa amekutwa na
umauti....
‘Poleni sana wanamuziki wa Malaika
Band kwa kuwa na wakati mgumu sana leo kwa kuomboleza kifo cha mwenzenu
wakati huo huo mnatakiwa muwaburudishe washabiki wenu huku wakiwa
wametia kilevi kichwani...
Hata
hivyo Totoo Ze Bingwa alimfahamisha kuwa kwa vile msiba umetokea jioni
huku maandalizi yote ya show yakiwa yamekamilika na ukizingatia kuwa
onyesho limekodiwa, basi hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuendelea
na show.
Totoo anadai kama msiba ungetokea mapema zaidi, basi wangeahirisha onyesho.
Adaya Nzinga aliitumikia Watoto wa Tembo ya Ndamndaa Cossovo kabla ya kutua Malaika miezi michache iliyopita.
Hisia imeelezwa kuwa katika nyimbo za Malaika zilizoko studio, marehemu Adaya Nzinga ametupia sauti kwenye nyimbo mbili.
إرسال تعليق