Meneja
wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani), kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo safari
ya timu ya Taifa ya watoto waendesha mitumbwi inayoelekea nchini
Morocco kushiriki mashindanoya wakimbiza mitumbwi mwezi ujao.
Na Mwandishi wetu
Tigo
Tanzania imetangaza udhamini wake kwa timu ya taifa ya watoto wadogo
waendesha mitumbwi, timu ambayo inaundwa na mabaharia watoto 10
waliochaguliwa na shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania
(TODA). Timu hii ya Taifa itashiriki mashindano ya 12 ya wakimbiza
mitumbwi wadogo Afrika yatakayofanyika Agadir, nchini Morocco kuanzia
tarehe 10 mpaka 18 Oktoba 2014.
Kukimbiza
chombo hiki ni zoezi la kuendesha mtumbwi mdogo, kwa kawaida si zaidi
ya urefu wa mita 6. Boti hii ya watoto wadogo ina urefu wa mita 2 na
inafaa kwa ajili ya watoto wa chini ya umri wa miaka 16.
Meneja
wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha alisema kuwa udhamini huu wa Tigo
ni sambamba na dhamira ya kampuni hiyo kuwekeza katika kukuza vipaji
vya wanamichezo nchini kuanzia wenye umri mdogo.
“Michezo
inatambuliwa kama jambo muhimu si tu katika maendeleo ya vijana lakini
pia katika kuunganisha vijana kutoka asili tofauti tofauti. Ni njia
muhimu sana katika kuongeza kujiamini na kujifunza ujuzi upya. Ni
makusudio yetu kuendeleza jitihada hizi za kuhamasisha mazingira ya
michezo hapa Tanzania,” alisema Wanyancha.
Aliongeza,
“Tunaamini katika uwezo wa mchezo kuwawezesha vijana kutimiza malengo
yao muhimu maishani. Sekta ya michezo inajenga fursa nyingi za ajira kwa
vijana ambao wanatamani kutumia vipaji na ujuzi wao ili kuleta
mabadiliko chanya katika maisha yao.”
Mwakilishi
wa nchi wa Shirikisho la mitumbwi midogo ya watoto Tanzania (TODA),
Nelly Coelho, alieleza kuwa uendeshaji wa mitumbwi hii ya watoto ni
mahsusi kwa ajili ya mabaharia vijana wenye umri kati ya miaka 8-15.
Meneja
wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akipiga picha ya pamoja na
Timu ya Taifa ya watoto mabaharia waliochaguliwa na shirikisho la
mitumbwi midogo ya watoto Tanzania(TODA) itakayoshiriki mashindano ya
wakimbiza mitumbwi yatayofanyika Agadir Morocco kuanzia tarehe 10 hadi
18 oktoba mwaka huu, Tigo ndio mdhamini wa safari hiyo.
Aliongeza
kusema, “Mabaharia waliofuzu wamekuwa wakipewa mafunzo kwenye ukingo wa
bahari wa Msasani kutoka chama cha wamiliki wa majahazi, Dar es Salaam.
Wengi wao walishawahi kushiriki katika mashindano mawili yaliyopita ya
Afrika chini ya ufadhili wa Shirikisho la Mabaharia kwa kushirikiana kwa
msaada wa vifaa vilivyotolewa na chama cha wenye Majahazi Dar es
Salaam, ambao TODA inatoa shukrani nyingi kwao .”
Msaada
wa Tigo umekuja kwa wakati mwafaka ambapo TODA ina mikakati ya
kutangaza mbio za vyombo vya majini kama njia ya kuendeleza vijana.
Mwakilishi wa TODA nchini amewashukuru Tigo kwa msaada huo na kuhimiza
ushirikiano huo uwe endelevu.
Mashindano
ya 12 ya watoto Afrika yameratibiwa kwa ushirikiano wa Shirikisho la
Royale Marocaine de Voile na Shirikisho la kimataifa la Mitumbwi ya
Watoto (TODA). Mashindano yatazileta pamoja nchi 13 barani Afrika ili
kushindana kwa ajili ya michuano hiyo. Kila nchi mwanachama katika
Afrika watapeleka mabaharia wapatao 10, waliofuzu katika majaribio ya
Taifa. Pia TODA wanahamasisha kuwa kati ya hao mabaharia 10 katika timu
angalau 3 wawe mabaharia wa kike ili kuhamasisha ukuaji wa vikosi kazi
kwa wasichana. Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kupeleka wawakilishi
wake kwenye tukio hili la kila mwaka kupitia Shirikisho la Mitumbwi
midogo Tanzania (TODA). Tukio hilo lilifanyika mwaka 2005 na 2012,
kwenye chama cha wamiliki wa Majahazi Dar es Salaam. Watoto watakaoenda
nchini Morocco ni Alexandra Pennanen Kok(13),Savanna Desmarguest(13),
Casey Deetlefs(12),Said Mkomba(13)
Hassan Mustafa(14), Vedastus Alphonce(14), Max Pennanen Kok(14), Friso Grolleman(12), Karim Jumanne(11) na Lenno Telemons(12).
Meneja
wa mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha akiongea na Timu ya Taifa ya
watoto mabaharia waliochaguliwa na shirikisho la mitumbwi midogo ya
watoto Tanzania(TODA) itakayoshiriki mashindano ya wakimbiza mitumbwi
yatayofanyika Agadir Morocco kuanzia tarehe 10 hadi 18 oktoba mwaka huu,
Tigo ndio mdhamini wa safari hiyo.
Watoto mabahria wakiwa kwenye mazoezi na mitumbwi yao maeneo ya slipway kujiandaa na safari ya nchini Morocco mwezi ujao.
Mtoto
baharia Max Pennanen Kok akionesha uhodari wake wa kuendesha mtumbwi
kwenye fukwe za bahari ya Hindi maeneo ya Yatch club mtoto huyo ni mmoja
ya watoto kumi watakaoshiriki mashindano ya wakimbiza mitumbwi nchin
Morocco mwezi ujao, Tigo ni wadhamini wa safari hiyo.
Post a Comment