TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 10.10.2014.
- MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA AKIWEMO MGANGA WA KIENYEJI KWA TUHUMA ZA KUPIGA RAMLI CHANGANISHI.
- MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA TETE WILAYA YA CHUNYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
MOJA LA JUMA, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA YA JAPHET SANGA (31)
MKAZI WA KITONGOJI CHA CHAPAKAZI – MBALIZI NA KUIBA TV, KING’AMUZI NA
DECK VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA TSHS. 350,000/=.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO MAENEO YA MLIMA RELI – MBALIZI,
KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA
MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:45 ALIVAMIA NYUMBANI KWA JAPHET SANGA NA
KISHA KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA HIYO NA KUIBA VITU HIVYO NA NDIPO
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIFANYWA NA HATIMAYE KUKAMATWA NA KUNDI LA
WANANCHI WALIOANZA KUMPIGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – MBALIZI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA. AIDHA, ANATOA RAI KWA WANANCHI KUJENGA TABIA YA KUWAFIKISHA
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAWEZE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MGANGA WA KIENYEJI ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA MUSSA SIWELU (27) MKAZI WA MBALIZI ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPIGA RAMLI NA KUSABABISHA TISHIO LA
MAUAJI KATIKA TARAFA YA MSANGANO, WILAYA YA MOMBA.
MGANGA HUYO ALIKAMATWA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO KATIKA KIJIJI CHA NTUNGWA, KATA YA
CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
AIDHA, KATIKA TUKIO HILO WATU
WATANO AMBAO WANADAIWA KUMLETA MGANGA HUYO KIJIJI HAPO PIA WANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. FRANK SILUNGWE (28) 2. JUMA JIPSON (35)
3. LOTO JULIUS (16) 4. GERVAS JIPSON (44) NA 5. LOCK MARKO (26), KYUSA
WOTE WAKAZI WA NTUNGWA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA
TETE AITWAYE YUSTA CREDO (36) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
09.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA TETE, KATA
YA KANGA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA
NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment