Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Kikosi cha wachezaji 18 na
viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam
tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa
Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Benin ambayo
imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu)
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati
tofauti.
Kikosi hicho kitafanya mazoezi
yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa
Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka
huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioko kwenye kikosi
cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza),
Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du
Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi
D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura,
Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve Mounie (Montpellier,
Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan
Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David
Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab
Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie
Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi
(Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou
Mama (Aspac, Benin).
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa
Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na
waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika
saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) katika Jengo la PPF Tower.
FDL YAANZA KUTIMUA VUMBI
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 11 mwaka
huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma,
Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya
Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati
Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na
Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana
kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam.
Kundi B ni Panone itaikabili
Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na
Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara
na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma).
Mechi nyingine ni kati ya Toto
Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza
na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment