Watanzania
kunufaika na kile ambacho wachambuzi huona kama nafasi adimu katika
sekta ya afya. Hii ni kwasababu nchi inatarajia kupokea wataalamu wawili
kutoka taasisi mashuhuri ya matibabu duniani. Kwa kushirikiana na
madaktari kutoka hosipitali ya Hindu Mandal. Madaktari kutoka hospitali
ya Apollo watahudumia na kutoa ushauri kwa wagonjwa wa figo na mfumo wa
mkojo siku ya Oktoba 10 na Oktoba 11 katika Hospitali ya Hindu Mandal
Dar es Salaam.
Watanzania
wengi wenye maradhi hayo hushindwa kupata matibabu hapa nchini na
badala yake husafiri nje ya nchi kwa ushauri na matibabu. Lakini kwa
sasa wanaweza kupata huduma hiyo hapa Tanzania katika hosipital ya
Hindu Mandal. Madaktari hao wawili kutoka hosipital inayoongoza katika
kutoa huduma bora duniani ya Apollo wanatarajia kutoa huduma iliyo na
ubora uleule hapa nchini Tanzania. Watanzania watapata fursa ya kuonana
na madaktari kati ya saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 8 kamili mchana
siku ya Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa 10 kamili jioni mpaka saa 1 na
nusu usiku kwa gharama ya shilling 45,000 tu kwa kila mgonjwa kwa ajili
ya kumuona dokta.
Ujio
wa Dk. Sanjay Maitra na Dk.Rajagopal katika hosipital ya Hindu Mandal
ni sehemu ya nia ya dhati ya hospitali ya Apollo ya kutoa huduma bora
za matibabu kwa wote na kujenga uhusiano mzuri na nchi ya Tanzania ambao
ulianza zaidi ya miaka kumi iliyopita. Madaktari hawa wakiwa Tanzania
watakuwa kuwawafuatilia wagonjwa mbalimbali, kupitia upya kesi za
magonjwa yao na kutoa ushauri juu ya matibabu kama taarifa za matibabu
zinavyoeleza.
Hatua
hii ni sehemu mpango mkakati wa hospital za Apollo wa kutokomeza
magonjwa kama haya nchini Tanzania. Hatua hii imechukuliwa kutokana na
utafiti uliofanyika hivi karibuni. Kulingana utafiti uliofanywa na
Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2011 vifo vitokanavyo na ugonjwa wa
figo nchini Tanzania vimefikia 4533 sawa na 1.03 asilimia ya vifo
vyote. Takwimu hizi zimeiweka Tanzania katika nafasi ya 54 duniani.
Ugonjwa wa figo umeripotiwa kuwa katika asilimia 14 miongoni mwa watu
wazima katika hospitali kulingana ujumla idadi ya watu. Chanzo cha kifo
kwa wagonjwa hao ni kushindwa kwa figo na mishipa ya moyo au matatizo
yanayojitokeza kutokana na ugonjwa huo. Katika utafiti mwingine
uliofanyika hivi karibunina Shirika la Afya Duniani WHO mwaka 2012
nchini Tanzania. Wagonjwa 100 waligundulika kuwa na magonjwa sugu ya
figo kutoka jumla ya wagonjwa 1,476 waliokuwa na magonjwa mbalimbali,
asilimia 61 walikuwa wanaume ambapo kati yao asilimia 91 walikuwa katika
ugonjwa sugu wa figo katika hatua ya nne na tano.
Dk.
Sanjay Maitra ni mtaalamu wa magonjwa ya figo. Anatarajia kuhudumia
watanzania wenye matatizo hayo katika kuwepo kwake nchini Tanzania.
Amefanikiwa katika upandikizaji wa figo kwa watu zaidi ya 500
uliofanyika chini ya usimamizi wake. Hivyo basi ana uzoefu mkubwa sana
katika masuala ya figo.
Mtaalamu
wa mfumo wa mkojo na viungo vya uzazi kwa wanaume, Dk.Rajagopal
atakuwa akihudumia wagonjwa wenye matatizo yanayohusiana na hayo kwa
kulenga zaidi katika upasuaji na matibabu. Wagonjwa wanaohitaji
Matibabu au ushauri juu ya jiwe katika figo, uhadubini, kufeli kwa
kibofu cha mkojo, matatizo ya mfumo wa mkojo, upandikizaji wa figo,
utasa, ukosefu wa nguvu za kiume, maambukizi ya kawaida au matatizo
mengine yanayohusiana na mfumo wa mkojo na viungo vya uzazi kwa wanaume
wanashauriwa kutokosa fursa hii iliyopo mbele yao.
Katika
kiliniki hiyo ya siku 2, wagonjwa watapimwa ili kugundua hali yao na
kushauriwa kama wanaweza kupata dawa na tiba ndani ya nchi ambayo
itasaidia kuponya maradhi yao. Kwa upande mwingine, kulingana na ukali
wa hali ya mgonjwa, watakuwa wanashauriwa kutafuta matibabu zaidi
ikibidi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya figo
kutokana na ukosefu wa kituo cha matibabu ya figo nchini Tanzania.
Gharama ya kusafirisha wagonjwa wa hali hii nje ya nchi si tu ghali kwa
serikali bali hata kwa wagonjwa wenyewe hukosa fedha za kutosha
kuwawezesha kupata tiba bora nje ya nchi. Hivyo kliniki hii ya siku
mbili kupitia madokta hawa ni baraka kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo
na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo ambao hawawezi kumudu
kusafiri nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Bw.
Radhey Mohan, Makamu Rais wa Shirika la kimataifa la Maendeleo ya
Biashara ndiye anayewezesha kliniki hiyo katika hospitali Hindu Mandal.
Post a Comment