Ajali ya lori na basi tanga yaua 12

Picha Na:- Maktaba
WATU 12 wamekufa papo hapo na wengine 19 wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria aina ya Toyota Costa inayosafiri kati ya Tanga na Lushoto kugongana na lori la mizigo aina ya Scania iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Juma Ndaki ajali hiyo imetokea leo eneo la Mkanyageni majira ya saa 1 asubuhi wakati magari hayo yakijaribu kupishana.
Alisema ajali hiyo ilihusisha coster yenye namba T 410 BJD iliyokuwa ikiendeshwa na Bakari Musa na lori lenye namba za usajili T 645 LBJ lenye tela namba T 605 ABJ lililokuwa likendeshwa na Benjamin Abeid.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Aisha Mahita akizungumzia ajali hiyo alisema maiti na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali Teule ya wilaya la Muheza.
Hata hivyo Dk. Mahita alisema majeruhi waliopokelewa katika Hospitalini hapo  Teule ni 25 ambapo kati yao 19 ni wanaume na 6 ni wanawake

Post a Comment

أحدث أقدم