Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
imesisitiza kuwa fedha zilizochukuliwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow
Sh306 bilioni ni za umma na waliohusika katika sakata hilo wachukuliwe
hatua kali na za kinidhamu.
Akihitimisha mjadala huo uliochangiwa na wabunge
35 na wawili kwa njia ya maandishi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto
Kabwe alisema fedha hizo ni mali ya umma na hilo limethibitishwa na
ofisi nyeti za Serikali.
Zitto alizitaja ofisi hizo kuwa ni Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“CAG, Takukuru na TRA kwa viapo ambavyo
hawatahojiwa sehemu yoyote, walikubali kwamba fedha hizo ni za wananchi,
sasa anayesimama na kupinga anatoa wapi mamlaka hayo.”
“Lakini huyu Profesa Muhongo alipoingia katika
wizara hii, alikuta Tanesco wanapata hasara ya Sh43 bilioni kwa mwaka,
lakini Desemba 2012 walipata hasara ya Sh117 bilioni na mwaka 2013
walipata hasara Sh467 bilioni, hii inaonyesha miaka mitatu imepata
hasara mara nne zaidi na huyu ndiyo Profesa Muhongo,” alisema Zitto.
Filikunjombe
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema
swali la kwanza ambalo CAG aliulizwa na kamati hiyo kuwa fedha hizo ni
za nani?
“Ndiyo maana sisi tulimuuliza na CAG hakupindisha
na alikuwa msafi kwa hili kuwa fedha ni za umma. “CAG, Takukuru, TRA
wote hawa ni watendaji wa Serikali na wamekiri kuwa ni fedha za umma,
sasa nashangaa hapa mtu anasimama na kupinga,” alisema Filikunjombe
ambaye pia ni Mbunge wa Ludewa (CCM).
Alisema kwa miaka 11 Tanesco walikuwa wakisema
fedha ni za kwao, lakini mwaka wa 12 kikao kimoja pekee wakasema fedha
siyo za kwao, hapo hakuna ukweli wowote.
“Kamati ya PAC siyo ya Zitto, siyo kamati ya
upinzani ni kamati yetu sote... tumewaonea watu wengi sana na mimi
nikipitapita huko magari ya Tanesco yote yana namba SU sasa sijui fedha
zao ni mali ya nani,” alihoji Filikunjombe.
Dk Kigwangalla
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla
alisema ukubwa wa Bunge katika Bunge hilo wakati tunafanya uamuzi, CCM
watatawala na kila kitu kutokana na wingi lakini hilo tutalifikia endapo
tutaweka mbele na kuthamini ukubwa wa Bunge hili.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق