
Siku chache baada ya mazishi ya kipa na nahodha wa timu ya taifa ya
Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa kuzikwa baada ya
kuuwawa na majambazi mchezaji mwingine wa timu ya taifa ya Afrika kusini
amevamiwa na majmbazi nyumbani kwake .
Majambazi watatu ambao bado hawajafahamika walivamia nyumba anakoishi
kiungo mshambuliaji wa Bafana Bafana Sibusiso Vilakazi ambako walipora
vitu kadhaa vya thamani .
Kwa mujibu wa ripoti iliyothibitishwa na mchezaji mwenyewe ,
majambazi hao walivamia nyumba ambamo mchezaji huyo anaishi na wanae na
walimuulizia mchezaji huyo kana kwamba wanataka kumdhuru.

Hata hivyo wazazi wawili wa Sibusiso waligoma kutaja mahali ambako
mchezaji huyo alikuweko hali iliyowafanya majambazi hao kuondoka bila
kumdhuru mtu yoyote .
Wakati mkasa huu ukitokea Vilakazi alikuwa amelala usingizi kwenye
nyumba iliyoko hatua chache toka iliko nyumba iliyovamiwa na hakutambua
chochote kilichokuwa kinaendelea hadi aliposimuliwa asubuhi yake .
Vilakazi ambaye ni nahodha wa klabu ya Bidvest Wits ameelezea
kusikitishwa kwake na tukio hilo hasa ukizingatia kuwa bado hajasahau
kilichomkuta mchezaji ambaye alikuwa akilala naye kwenye chumba kimoja
kwenye kambi ya timu ya taifa Senzo Meyiwa .
إرسال تعليق