Alisema njia pekee ya kulimaliza suala hilo
linalotarajiwa kuwasilishwa bungeni leo, ni kwa wabunge kuijadili
taarifa hiyo na kuchukua hatua zinazostahili.
Mama Nyerere alisema hayo jana nyumbani kwake
Msasani Dar es Salaam, alipojibu maswali ya waandishi wa habari
waliotaka kujua maoni yake kuhusu escrow kama suala hilo linatakiwa
kujadiliwa au kutojadiliwa bungeni. “Jambo hili sasa liko kwenye
magazeti kwa muda mrefu, ningependa lijadiliwe na wabunge limalizike
kabisa, lisipojadiliwa tutatafuta matatizo makubwa baadaye,” alisema.
Mama Nyerere alisema suala hilo linagusa masilahi
ya umma, hasa katika kipindi hiki ambacho wengi wanakosa huduma muhimu
kutokana na uhaba wa fedha unaoikabili Serikali.
“Wanaposikia ripoti za ukaguzi zinafichwafichwa
wakati ndugu zao wanakufa kwa kukosa dawa ni lazima watakuwa na hasira
na baadaye kusababisha machafuko,” alisema.
Hata hivyo, alisema katika Serikali ya Awamu ya Kwanza kulikuwa na wizi wa mali ya umma lakini hali iliyopo sasa ni ya kutisha.
“Wizi haujaanza leo, hata zamani watu walikuwa
wanasogeza fedha za umma, lakini sasa hivi hali imezidi kwenye vyombo
vya habari kila siku ni ufisadi, jambo muhimu ni kuchukua hatua haraka,”
alisema.
- Mwananchi.
- Mwananchi.
Post a Comment