| Chama cha Republican kimepata idadi kubwa ya viti katika baraza la Seneti. |
Na RFI
Nchini Marekani chama cha
Republican kinaelekea kupata idadi kubwa ya viti katika bunge la Senate,
na sasa wanahitaji viti sita tu ili kudhibiti bunge hilo.
Matokeo ya awali yanaonesha kuwa
chama hicho kimepata ushindi katika majimbo ya Arkansas, Montana, South
Dakota na West Virginia.
Kulingana na matokeo ya awali, chama cha Republican kinaongoza kwa viti 51 kwa jumla ya viti 100.
Kiongozi wa chama cha Republican
Mitch McConnell, amehifadhi kiti chake katika jimbo la Kentucky na
kusema mambo yanavyokwenda inaonesha wazi kuwa raia wa Marekani wana
imani na chama cha Republican.
Chama cha Republican pia
kimepata ushindi katika majimbo ya Mississippi, Alabama, Maine na South
Carolina, huku chama cha rais Barrack Obama Democratic kikiibuka ushindi
katika majimbo ya Massachusetts, Rhode Island, Delaware , New Jersey na
New Hampshire.
Ikiwa chama cha Republican
kitashinda viti vingi, inaaminisha kuwa itakuwa vigumu kwa miswada ya
serikali kupitishwa katika baraza hilo la Seneti.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق