Na Julius Kithuure, Nairobi
Huku Wakenya wanaposhughulika na hali ngumu ya mauaji ya watu wengi ya
hivi karibuni ya maofisa polisi yaliyofanywa na majambazi katika kaunti
za Turkana na Baringo, wito wa kujiuzulu kwa walio katika nafasi za
uongozi za masuala ya usalama wa taifa umeongezeka.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya
David Kimaiyo na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na
Uratibu wa Serikali ya Taifa Joseph Ole Lenku wakiwa wamesimama kwenye
kituo cha uhakiki tarehe 9 Aprili. [Tony Karumba/AFP]
Mashambulio ya kuvizia ya mwishoni mwa wiki katika kaunti ya Turkana
yamefuatia baada ya wiki ya mashambulio madogo ya hapa na pale dhidi ya
maofisa polisi na raia ambayo yaliua maofisa polisi wapatao 21 na raia
watatu, yakiwajeruhi wengine kadhaa, na kuharibu mali za watu binafsi na
polisi.
Jumamosi mchana (tarehe 1 Novemba), majambazi wenye silaha nzito
walishambulia lori lililokuwa limewabeba maofisa polisi kati ya Kapedo
na Lokori. Polisi hao walikuwa katika kazi maalumu ya kuchukua mabaki ya
gari lililochomwa moto la Kitengo cha Huduma za Jumla (GSU) ambalo
lilishambuliwa katika eneo hilo hilo wiki iliyotangulia, ambapo maofisa
polisi watatu na raia watatu akiwemo mwalimu waliuawa.
Katika tukio tofauti Jumapili asubuhi sana, takribani wanaume dazani
waliokuwa na silaha aina ya mapanga walijaribu kushambulia kambi ya
maaskari jeshi huko Nyali, karibu na Mombasa. Askari waliokuwa katika
jukumu la ulinzi walijibu mashambulizi, wakiwaua washambuliaji sita papo
hapo na wa saba wakati wakikimbilia kwenye msitu ulio karibu, na
mshambuliaji mmoja alikamatwa.
Askari mmoja alikatwa na panga wakati wa makabiliano, na alifariki
baadaye kutokana na majeraha aliyopata katika hospitali ya Pandya huko
Mombasa.
Genge lingine lenye silaha na mapanga pia lilijaribu asubuhi na mapema
Jumapili kushambulia kambi ya utawala ya Malindi. Maofisa polisi
walifanikiwa kuwazuia washambuliaji baada ya mapigano makali ya silaha,
ingawaje washambuliaji kwanza waliharibu baadhi ya magari yaliyokuwa
yameegeshwa katika kituo cha polisi.
Utokeaji wa mara kwa mara na uzito wa matukio hayo inaonyesha kwamba
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo na Waziri wa Ndani na Uratibu
wa Serikali ya Taifa Joseph Ole Lenku wamekosa udhibiti wa hali hii,
baadhi ya raia wamesema, wanatoa wito wa wawili hao kujiuzulu au
kuondolewa katika ofisi na Rais Uhuru Kenyatta.
Hali ya usalama 'isiyokubalika'
"Matukio haya yanaonyesha kwamba kuna kitu hakiko vizuri kuhusiana na
namna Lenku na Kimaiyo wanavyoendesha chombo hichi cha usalama, na muda
wa wao kutoka au kujiuzulu umewadia," alisema Robert Matano, mwenye umri
wa miaka 45, mmiliki wa mgahawa wa Karibu huko Nairobi.
Matano alisema alishangaa ni maisha ya watu wangapi zaidi yatapotezwa
kupotea kabla ya Kimaiyo na Lenku hawajachukua jukumu binafsi la
operesheni za polisi zilizovurugwa na mikakati isiyo na ufanisi.
"Kwa hakika rais anapaswa kwa sasa kujua kwamba watu hawa wawili
wanapaswa kuacha [haraka] kuongoza nafasi za juu wanazoshika," aliiambia
Sabahi. "Uhuru anapaswa kuwawajibisha na kwa hilo kuwafukuza kazi kama
wataendelea kung'ang'ania kukaa kwenye kazi zao."
Lenku na Kimaiyo hawajabadilisha mbinu zao za usalama licha ya mauji ya
watu wengi ambayo yametokea chini ya uangalizi wao, Matano alisema.
"Tulikuwa na shambulio la kigaidi la Wesgate Septemba [2013] ambalo
liliua watu wapatao 67, tarehe 15 na 16 ya mwezi Juni mashambulio huko
Mpeketoni mji ulio huko Lamu ambalo liligharimu maisha ya watu 63, na
sasa mauaji ya watu wengi ya maofisa polisi 21, pasipo kusahau mauji ya
hapa na pale katika sehemu mblimbali nchini," alisema. "Nani atajibu
kuhusu upotevu wa maisha haya na lini?"
Kiwango cha sasa cha usalama hakikubaliki, alisema mchambuzi wa masuala
ya usalama mwenye makaazi huko Nairobi Mwenda Mbijiwe, akiongezea kwamba
inaonekana kuwa serikali imeshindwa jukumu lake la kutoa usalama.
"Mashambulio ya ujasiri kwenye kambi ya maaskari jeshi hayakutokea kabla
katika nchi hii," aliiambia Sabahi. "Ni ishara wazi ya namna hali
isivyo na usalama katika taifa letu na namna uthubutu wa kufanya uhalifu
ulivyo."
Maandalizi zaidi yanahitajika
Polisi wahakupaswa kuwepo katika eneo hilo pasipo kufikia matarajio
katika tukio la hivi karibuni la huko Turkana kwa kuwa walipaswa kufanya
upelelezi kuhusu eneo hilo na hatari zake na kuandaa mpango wa
kitaalamu kushughulikia kitisho chochote kinachoweza kutokea, Mbijiwe
alisema.
"Ni wazi kuwa hawakuwa wamejiandaa, ambayo kwa bahati mbaya inamanisha
hawakujifunza chochote kutoka Novemba 2012 operesheni Baragoi ambayo
maofisa polisi 42 walishambuliwa na kuuawa na majambazi katika kazi
maalumu ya kurejesha mifugo iliyokuwa imeibiwa," alisema.
Wakati wahalifu wanaposhambulia vikosi vya usalama na kuua wengi
miongoni mwao kwa tukio moja, inaonyesha hakuna aliye salama, alisema
msimamizi wa zamu wa Kampuni ya Viatu ya Bata Margaret Maina, mwenye
umri wa miaka 32, huko Nairobi.
"Kama polisi hawawezi kujilinda wao wenyewe, hivyo nani atatulinda
sisi?" alisema, akielezea shambulio hilo kama fedheha kwa idara ya
polisi.
"Kimaiyo anapaswa kuwaheshimu na kuwathamini maofisa wa ngazi za chini
waliouawa wakiwa kazini kwa kukamilisha siku, ili kwamba rais awe na
nafasi ya kumteua mtu mwingine mwenye uwezo wa kushawishi imani katika
yombo vvya usalama," aliiambia Sabahi.
"Tumekuwa wavumilivu kwa huduma dhaifu za Lenku na Kimaiyo kwa kadiri ya
muda mrefu," alisema Justus Muketha, mfanyakazi mstaafu wa benki mwenye
umri wa miaka 60, akieleza kamba watu hao wawili walifanya "kuzungumza
mambo mazito na kutoa tarehe za mwisho ambazo kamwe hazijawahi kufuatiwa
na vitendo".
Muketha aliwakanusha watu hao kwa utaratibu wao wa "kushtukiza" katika
usalama na kutoa wito wa kuacha kazi haraka "kwani mambo yamepita
kiasi".
Alichukulia suala hilo pamoja na ushughulikiaji wa rais katika tukio
hilo, akisema kuna ushahidi mdogo unaoonyesha hadhari ya Kenyatta ya
wiki iliyopita kwamba "hatua kali" zingechukuliwa dhidi ya wale
waliohusika na mashambulio imetekelezwa au washambuliaji hao
wamesikiliza tahadhari yake.
Kuwajibika kwa kushindwa kwa usalama
Mwenyekiti wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Sera (IPOA) Macharia Njeru
alisema kukosekana kwa maandalizi na uratibu mzuri wa muundo wa kikosi
cha polisi kwa sehemu ni kitu cha kulaumiwa kwa kutokuwepo kwa usalama.
Katika Mkutano na Vyombo vya Habari Jumatatu, Njeru alisema Kimaiyo na
Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi Ndegwa Muhoro wanapaswa kuwajibika kwa
shambulio la maofisa polisi, kuomba radhi kwa umma na kuacha kazi badala
ya kutafuta sababu.
"Kufanikiwa kwa mamlaka kumethibitisha kwamba kuwepo kwa sera zenye
ufanisi kunahitaji mkakati thabiti na maandalizi ya mipango ya mwaka
ikiwa ni pamoja na changamotoo za usalama na vipaumbele vinavyozingatia
hali iliyopatikana katika mikoa tofauti," alisema Njeru.
Alibainisha taarifa ya hivi karibuni ya IPOA katika shambulio la
Mpeketoni, akisema Kimaiyo anapaswa kutekeleza mapendekezo ya kuzuia
matukio ya siku zijazo, kama vile mauaji ya Kapedo.
Julius Njuguna, mwenye umri wa miaka 44, ambaye ni msimamizi wa ulinzi
wa Duka kubwa la Ridgeways huko Nairobi, alisema mashambulio ya hivi
karibuni yaliacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu na muda wa
kuwauliza ni sasa.
"Kwa nini kikundi kidogo cha maofisa waliokuwa wamejiandaa bila kuwa na
mpango wowote wa usaidizi walipelekwa katika kaunti ya Turkana, eneo
linalofahamika kwa ujambazi, kisha siku kadhaa mapema, gari la GSU
lilikuwa limetekwa na majambazi watatu na maofisa watatu waliuawa?"
alisema. "Kwa nini kulikuwa hakuna kikosi cha kuwasaidia katika
operesheni hiyo ya hatari?"
"Wakati maisha ya maofisa waliokuwa hawana taarifa yalipopotea katika
mazingira hayo ya kizembe, maofisa wa ngazi ya juu katika usalama
walipaswa kuwajibika na kuchukuliwa hatua za muhimu dhidi yao,"
aliiambia Sabahi.
Katika mazingira hayo ya sasa, mhitimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha
Nairobi Bernice Gathoni, mwenye umri wa miaka 39, alisema anatarajia
Kimaiyo na Lenku kuachia nafasi zao.
"Kuchukua udhaifu wa mtu mwingine ni dalili ya uhodari wa kuendesha
shughuli za serikali," aliiambia Sabahi. "Inaonyesha heshima kwa
waliofariki, familia zao, marafiki na taifa kwa ujumla."
Wito wa utulivu, kuungwa mkono
Hata hivyo, Jonahathan Kibugi, muuzaji wa bima za maisha mwenye umri wa
miaka 39 huko Nairobi alisema ilkuwa ni hali ya kutokomaa kudai viongozi
wa usalama kuachia madaraka.
"Polisi wetu wameshafanya shughuli nyingi za uhalifu na ugaidi lakini ni
Wakenya wachache tu waliotoa maoni kwa inspekta jenerali kwa hili,"
aliiambia Sabahi. "Tumpeni muda kufanya huduma ya polisi ya kisasa na
kisha tutamhukumu kwa lile atakalokuwa amelikamilisha mwishoni mwa mwaka
ujao."
Msemaji wa Polisi Zipporah Mboroki pia aliwaomba raia kuwa watulivu.
"Inspekta jenerali alianzisha kampeni nyingi za kuboresha operesheni za
polisi na uwezo wao wa kukabiliana na tatizo," aliiambia Sabahi.
"Matokeo haya hayawezi kuonekana. Anahitaji muda na kuungwa mkono na
Wakenya wote ili aweze kukamilisha ahadi zake."
"Akitoa wito wa kuacha kwake kazi kila mara huduma ya taifa ya polisi
inakabiliwa na changamoto ni kutokuwa na uaminifu," alisema.
Chanzo: sabahionline.com
إرسال تعليق