SAKATA LA TEGETA ESCROW, WABUNGE WAKINUKISHA BUNGENI

Naibu Spika wa Bunge, Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la".
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, "Punguzeni jazba", akiwasihi wabunge kuwa serikali iko makini na inasubiri kwa hamu taarifa hiyo ili kila mtu hata yeye akibainika abebe msalaba wake, lakini akatahadharisha kuhusu umuhimu wa kuheshimu mihimili ya dola ikiwemo mahakama.
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, (CHADEMA), akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, wakati lile sakata la IPTL, linalogubikwa na akaunti iliyojichukulia umaarufu TEGETA ESCROW, lilipoibuka wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu. Wabunge wanataka "ngoma" ijadiliwe bungeni, licha ya kashfa hiyo kuwa tayari Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mbunge wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, huyu ndiye aliyeibua kashfa ya akaunti ya Tegeta-Escrow.
Mbunge wa Iringa mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa akitoa mwongozo.
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akichangia.
Mbunge kijana, Esther Bulaya, (CCM) naye akichangia kuhusu kujadiliwa ripoti hiyo.
Mbunge wa Longido,(CCM), Lekule Laizer akichangia mada.


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo, (CCM), Samwel Sitta akitoa hoja.
Mbunge wa Kasulu mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ndiye aliyemchokoza Waziri Mkuu kuhusu ripoti hiyo kujadiliwa bungeni.
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli naye akichangia.
(Picha kwa hisani ya K-VIS Production)

Post a Comment

Previous Post Next Post