Straika mpya Simba mfungaji bora Kenya

Mganda Dan Sserunkuma
Mchezaji anayetajwa kwenye orodha ya nyota wanaotarajiwa kumwaga wino Klabu ya Simba, Mganda Dan Sserunkuma, ameng'ara katika tuzo za Ligi Kuu ya Kenya zilizotolewa jijini Nairobi, Kenya usiku wa kuamkia jana.
Kwa mujibu wa Mtandao wa futaa.com, kiungo wa Sofapaka, Anthony Ndolo alitwaa mataji mawili makuu; mchezaji na kiungo bora wa mwaka huku kocha wake Mganda Sam Timbe akimaliza wa pili nyuma ya Mike Mururi wa Chemelil Sugar katika kipengele cha kocha bora.

Mabingwa Gor Mahia kwa upande wao walijivunia ushindi wa David Owino na Ronald Ngala kwenye safu ya beki bora na mwenyekiti bora wa klabu na kisha timu hiyo kuibuka ya pili kwenye timu yenye nidhamu (mchezo wa kiungwana) msimu huu.

Kiungo wa Gor na Timu ya Taifa ya Uganda (Cranes), Geoffrey Kizito naye alitangazwa namba mbili katika tuzo za kiungo na mchezaji bora huku mlinda mlango Jerim Onyango akimaliza wa pili kwenye tuzo za kipa bora wa mwaka, nyuma ya Jairus Adira wa Chemelil Sugar.

Kwenye tuzo nyingine, Sserunkuma ambaye mwaka jana alikuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Kenya, alitwaa taji la daluga la mfungaji bora kwa kucheka na nyavu mara 16 msimu huu.

TUZO ZA WACHEZAJI/ MAKOCHA/VIONGOZI BORA 2014
Mchezaji Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka), Kipa Bora: Jairus Adira (Chemelil Sugar), Beki Bora: David Owino (Gor Mahia), Kiungo Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka), Mfungaji Bora: Dan Sserunkuma (Gor Mahia).
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post