Mkataba wa Izuchukwu waipasua kichwa Simba SC

Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mnigeria, Emeh Izuchukwu(mwenye jezi ya bluu)
Na Wilbert Molandi
BAADA ya Kamati ya Usajili ya Simba kulipitisha jina la mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mnigeria, Emeh Izuchukwu kwenye usajili wao, uongozi wao hivi sasa upo kwenye mipango ya kusitisha mkataba wake kwenye Klabu ya Eleverum inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Norway.
Simba ipo kwenye mipango ya usajili wakati huu wa dirisha dogo lililofunguliwa tangu Novemba 15, mwaka huu ikiwa ni mipango ya kuimarisha kikosi chao baada ya kuanza msimu kwa kuyumbayumba.Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimeeleza kuwa, tayari wameanza mazungumzo na Eleverum kwa ajili ya kuuvunja mkataba ili arejee Simba.
Kiliongeza kuwa, Simba wanaamini mazungumzo yao na klabu hiyo yatafikia pazuri na mshambuliaji huyo atatua kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo kabla halijafungwa Desemba 15, mwaka huu.
“Usajili wa Izuchukwu ni mgumu katika kumpata, licha ya mwenyewe kutaka kurejea kuitumikia timu yake ya zamani ya Simba, kwa sababu ili asaini Simba basi ni lazima mkataba wake tuusitishe kwenye klabu yake anayoichezea.
“Tupo kwenye mazungumzo na viongozi wa klabu anayoichezea ya Norway kwa ajili ya kuvunja mkataba alioubakisha wa kuitumikia Eleverum, mara tutakapomalizana haraka atatua nchini kwa ajili ya kuichezea Simba,” kilisema chanzo hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post