WAUMINI wa msikiti wa Masjid Ghadiri uliopo Kigogo
Post, jijini Dar es Salaam, leo wamefanya matembezi kuanzia Ilala mpaka
Kigogo, kwa ajili ya kuhimiza na kuhamasisha amani kwa Watanzania na
walimwengu kwa ujumla.
Tarehe 4 Novemba kwa Waislam inajulikana kama siku ya Ashura, siku
ambayo ilishuhudia moja ya mihanga adhimu na mikubwa ya wanadamu katika
kumbukumbu za kihistoria za kila mwaka.
Ni siku ambayo, mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Muhammad (S.A.W.) na
watu wa karibu yake waliuawa kikatili katika jangwa la Karbala nchini
Iraq na miili yao kukatwakatwa kwa amri ya Yazid bin Muawiyah, mtawala
dhalimu wa ulimwengu wa Waislam kwa wakati huo.Hayo yamesemwa na Shehe
Hemed Jalala, Imam wa Masjid Ghadiri Kigogo Post alipowaongoza mamia ya
waumini katika matembezi hayo.
Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com
إرسال تعليق