Watatu mbaroni kwa Dola bandia za milioni 19/-

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Frasser Kashai
Jeshi la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia Dola za Kimarekani 11,200 (Sh. milioni 19,214,160) Watuhumiwa hao ni pamoja na Julius Kanza (30), Kenedy Binagi (35) na Ramadhan Saddy (33), wote wakazi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Frasser Kashai, alisema ,watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17, mwaka huu saa 7.30 mchana katika eneo la Barabara ya 16, Kata ya Ngamiani, jijini hapa. Kamanda Kashai alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye gari.

Alisema katika mahojiano na Polisi, watuhumiwa hao walikiri kuwa ni wafanyabiashara wa fedha bandia na wamekuwa wakiziuza kwa muda mrefu.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa raia wema na ndipo tulipoanza kuwafuatilia na hatimaye kuwakamata wakiwa wamehifadhi fedha hizo ndani ya gari na katika mahojiano wamekiri kuwa wao ni wafanyabiashara wa muda mrefu,” alisema.

Alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم