WATU sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Hiace kugongana na gari lingine aina ya Toyota Coaster katika eneo la Uchira Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo zinasema kuwa, Toyota Hiace yenye namba za usajili T
118 ABP lilikuwa likitokea wilayani Mwanga kuelekea mjini Moshi, liligongwa ubavuni na Coaster lenye namba za usajili T925
BUX, lililokuwa likitokea Moshi kuelekea Mwanga.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa, Coaster lilipofika eneo la Uchira lilipasuka tairi la mbele na kuligonga ubavuni Toyota Hiace, iliyopinduka na kusababisha vifo vya watu sita.
Walisema ajali hiyo ambayo ilitokea Desemba 30, mwaka huu, saa 6:45 leo mchana, ilisababishwa na gari ya Coaster liliyokuwa likitokea Moshi mjini ambapo lilipasuka tairi la mbele na kukosa mwelekeo na kuligonga ubavuni gari dogo aina ya Hiace.
Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo Leo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hai, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema idadi kamili ya vifo haijafahamika, lakini taarifa za awali ni watu sita.
Alisema kuwa, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya KCMC, wakati majeruhi wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi na wengine wakiwa katika Hospitali ya KCMC.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba hawajapata taarifa kamili, lakini ikikamilika watatoa kwa
waandishi wa habari leo
إرسال تعليق