Dar/Zanzibar. Viongozi wa dini wamezidi kuikaba koo Serikali kuhusu kashfa ya Escrow na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wakitoa mahubiri katika ibada takatifu ya sikukuu
ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo juzi, viongozi hao wamewataka viongozi wa
Serikali kuwasaidia wananchi wao.
Askofu Augustine Shao wa Kanisa la Romani Katoriki
Jimbo la Zanzibar alisema zoezi la kura ya maoni ya kupitisha Katiba
mpya lisitishwe hadi wananchi watakapopewa elimu ya uraia ya kutosha
kabla ya kufanyika mwakani.
kipindi cha miezi minne iliyobakia kabla ya
wananchi kupiga Kura ya maoni akitoshi kutoa elimu ya uraia hasa kwa
kuzingatia asilimia 70 ya Watanzania wanaishi vijijini kusikokuwa na
huduma ya umeme na wengi wao wakiwa hawana nakala za Katiba
inayopendekezwa tangu kupitishwa na Bunge la Katiba Oktoba mwaka
huu.Askofu Shao alisema mwakani ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu pia wahusika
walitakiwa kuangalia hilo, lakini alisema iwapo wananchi watapatiwa
elimu ya kutosha wanaweza kufanya uamuzi wa msingi na kufanikisha kupata
Katiba yenye masilahi kwa taifa na wananchi wake.
Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la TAG
Zanzibar, Dickson Donald alisema kwamba Watanzania watapata Katiba bora
kama watapewa elimu ya uraia ya kutosha na zoezi lenyewe kufanyika kwa
uwazi bila ya mizengwe.
Alisema wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu
mwakani ni vizuri Watanzania kuchagua viongozi kwa kuwapima uadilifu na
uwezo badala ya kuangalia vyama na itikadi. Alisema kuwa vigezo hivyo
iwapo vitazingatiwa Taifa litapata viongozi bora na kufanikiwa kudhibiti
vitendo vya ufisadi na ubadhirifu na kuimarisha misingi ya utawala na
sheria.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible
Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe alisema CCM imeshikwa na hofu kuwa
upinzani unaweza kushika dola kupitia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Askofu
Kakobe alisema hofu hiyo ndiyo inayokifanya chama hicho tawala
kuikumbatia Tume ya Uchaguzi isiyokuwa huru na haki, kushindwa kuboresha
daftari la wapigakura na kupanga chaguzi zifanyike siku za Jumapili.
Katika hatua nyingine, aliwashangaa Ukawa kukubaliana kwenda kwenye uchaguzi mkuu ujao angali kuna tume isiyokuwa huru.
Aliongeza akisema Tume ya Uchaguzi iliyopo kwa
sasa bado ni kiini macho kutokana na viongozi wake kuteuliwa na
mwenyekiti wa CCM.
- Mwananchi
- Mwananchi

Post a Comment