Makamba: Waliochota Escrow wabanwe zaidi

Mwanza. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema watu wote waliohusika katika sakata la kuchukua Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wenye kutumia madaraka yao vibaya.
Akizungumza na vijana kutoka vyuo mbalimbali jijini Mwanza, Makamba alisema fedha zilizochukuliwa ni za umma na inapaswa waelewe kuwa kiongozi yeyote yupo kwa ajili ya kumsaidia mwananchi na si kumkandamiza.
Alimshukuru Mungu akisema kuwa ‘mvua hiyo ya manyunyu’ inawanyeshea wengine, yeye hausiki kwa lolote kuhusu fedha hizo. “Dalili ya ngozi au manyoya ni dhahiri kuwa kuna mnyama kachinjwa na waliohusika katika uchinjaji huo wawajibishwe kwa kufikishwa mahakamani,” alisema Makamba.
Alisema Taifa haliwezi kujengwa kwa wizi au udokozi na ili kusaidia Taifa ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe au itolewe adhabu ambayo itasaidia kukomesha wizi wa aina hii, ili na wengine nao wajifunze.
- Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم