Manowari ya Marekani
Wanamaji
kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita
kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za
Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson
inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya
tatu tangua kuanza msako dhidi ya ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa
kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za
Singapore, Malaysia ,Australia,Korea Kusini,Thailand na China
wanashiriki katika kazi hiyo. Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na utafutaji
ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli
30,ndege 15 na Helkopita katika eneo la tukio. Ndege hiyo ilipotea
ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa
na abiria 162. (BBC)
إرسال تعليق