Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Express ya Uganda, Francis Ntalazi amedai Simba ilitumia saini ya kughushi kupata mkataba wa Simon Sserunkuma kama mchezaji huru.
Ntalazi alilalamikia kitendo cha kughushi saini
yake katika mkataba wa mchezaji huyo kilichofanywa na mmoja wa viongozi
wa klabu hiyo.
“Ilinishangaza kwani hakuna mtu anayeruhusiwa
kusaini badala ya mtu mwingine bila idhini ya mhusika, ninapeleka suala
hili polisi na tayari nimeshawaelekeza mawakili wangu kufuatilia jambo
hilo,” alisema Ntalazi.
Pia, ameishauri Simba iende Uganda kuwasiliana na
kufanya mazungumzo halali kama wanamtaka mchezaji huyo kwani kwa mpango
waliofanya wamemchukua bure na kwa saini ya kughushi.
“Lakini sishangazwi na baadhi ya watu waliokuwa
wanajua jinsi mkataba ilivyokuwa, ninachotaka ni Shirikisho la Soka
Uganda (Fufa) kuingilia kati na haki itendeke,” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia
Hanspoppe alisema tayari Sserunkuma amepata Hati ya Uhamisho wa
Kimataifa (ITC) na wanategemea atarejea wakati wowote na kujiunga na
wenzake kwa ajili ya kujiandaa na ligi.
“Hatujasikia pingamizi lolote kutoka kwa uongozi
wa Express, mchezaji tumemsajili na alirudi Uganda kufuata ITC ambayo
tayari ameshaipata,” alisema.
Kwa mujibu wa kanuni za ITC, hakuna mchezaji
anayeruhusiwa kuifuata mwenyewe kwa sababu uhamisho hufanywa
kieletroniki na kuhusisha mashirikisho.
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema bado hawajapokea ITC ya Simon Sserunkuma
Post a Comment